Na Niccomeditz
KUTOKANA na mvua kubwa zilizonyesha karibu maeneo yote ya nchi na kuleta maafa hususan katika jijin la Dar es Salaam Kampuni ya Aqua Cool Ltd Watengenezaji wa maji safi ya Kisima Pure Drinking Water imetoa msaada wa mavazi ya kujikinga na mvua ya mpira (ponchos) kwa wakazi wa wilaya ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Msaada huo ulitolewa na uongozi na wafanyakazi wa kampuni hiyo kwa
makundi mbalimbali kama watembea kwa miguu, mama lishe , waendesha
bodaboda na wafanyabiashara wadogo wadogo maarufu kama machinga.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini wakati wa kutoa msaada huo
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hiyo Ali Dhanji alisema kampuni
imefanya hivyo kama sehemu ya shukrani kwa jamii, kuwajali wateja wao
pia kwa wananchi wa kawaida walioathirika na kutatizwa na kadhia
ya mvua inayoendelea kunyesha .
Aliongeza kusema wamefanya hivyo ili kuwarejeshea urahisi wa kufanya
shughuli zao ambazo kutokana na maafa yaliyosababishwa na mvua na
kuwakwamisha kuendelea na shughuli za kujipatia kipato kwa muda hivyo
kuyumba kiuchumi.
"Tusingependa kuona athari za mafuriko kushusha uchumi na shughuli
zenu kama ilivyokuwa mwaka jana , ndio maana tunaishukuru manispaa ya
Temeke kwa kuliona hilo mapema na kuboresha miundombinu ya barabara ya
changombe ili watu waweze kuendelea na shughuli zao za kawaida,"
alisema Ali.
Mfanyabiasha
mmoja akiendelea kufanya biashara yake bila wasiwasi huku akiwa
amevalia nguo ya kuzuia mvua wakati mvua ikiendelea kunyesha katika
maeneo ya Temeke jijini Dar es Salaam. |
Aidha aliongeza kuwa wamejizatiti wataendelea kusambaza takribani
mavazi ya kujikinga na mvua ya mpira (ponchos) 6000 katika maeneo
mengine ya jiji ndani ya wiki moja kwa kuzingatia kuwa faida ya
shilingi 20,000 anayoipata mtu kwa siku moja ni kubwa sana
ukilinganisha na gharama ya mavazi ya kujikinga na mvua ya mpira
(ponchos) moja ambayo ni shilingi 2000.
Aidha alisema msaada huo ni sehemu ya kutekeleza mradi wao wa KISIMA
CARES 2015 wa kurushirikisha wateja wake faida wanayoipata kutoka
kwenye jamii pamoja na kutoa misaada mingine kama maji ya kunywa na
malazi kwa yatima na walemavu katika maeneo mbalimbali ya jiji.
Kampuni ya Aqua Cool Ltd watengenezaji maji safi ya Kisima inatarajia
pia kutoa misaada kwa wananchi hususani vijana na ili waweze kuongeza
kipato na kuinua hali zao kiuchumi . Kwa maelezo tembea tovuti ya
kampuni : www.kisimawater.com au Facebook Page "Kisima Pure
Drinking Water.
No comments:
Post a Comment