Mashimozz katika barabara hii ya Migombani, inayotokea DriveIn (makao makuu ya Zantel) kuelekea Victoria (Kariruki Hospitali) mpaka Makumbusho jijini Dar es salaam, yamekuwa ni kero kwa watumiaji wa njia hiyo, hasa kutokana na ukubwa wa mashimozz yaliyopo kwenye barabara hiyo. huo mpishano wa vyombo vya usafiri hapo pichani, si kwamba unatokana na mbwembwe za madereva, la hasha ni kutokana na namna ya kuyakwepa mashimozz hayo yaliyosheheni katika barabara hiyo.


Hivi ndivyo hali ilivyo katika barabara hiyo hizi sasa, na hii ni kutokana na mvua zilizonyesha hivi karibuni. maana kabla ya hapo mambo yalikuwa mswano kabisa.

Hapa ni mwendo wa staili ya kinyonga, maana wenye kwenda mbio huku hakuwafai kabisa.


Kila dereva anaangalia sehemu yenye unafuu kwake ndio aweze pitisha gari yake.


Hii gari imekwama baada ya kunasa kwenye shimo la Chemba iliyofumuka kutokana na kuzidiwa na maji, hivyo hapo kuna shimo kubwa sana ambalo liko wazi.hivyo watumiaji wa njia hii kuweni makini sana na hapo maana haijulikani ni lini mkandarasi atapita na kuja kufanya mambo.

Utataribu wa kuichomoa gari hiyo ukaanza kutoka kwa watu waliokuwa kwenye msururu wa kuvuka eneo hilo korofi.


Msururu wa magari ukisibiri kupita kwenye eneo hilo ambalo ukikosea tu taimingi, imekula kwako.
No comments:
Post a Comment