HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, May 13, 2015

HAKUNA MAFUNZO KWA MADEREVA KILA BAADA MIAKA MITATU - MPINGA

Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii

KIKOSI cha Usalama Barabarani kimesema hakuna mafunzo au kutakiwa kwenda kusoma kutokana na mpango huo haujafika muda mwafaka.

Hayo ameyasema leo jijini Dar es Salaam,Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP),Mohamed Mpinga kuwa mpango huo wa madereva kwenda katika mafunzo na masomo ulikuwepo lakini sio kwa sasa kutokana na kutokuwepo kwa mitaala na vyuo vitakavyofundishwa.

Mpinga amesema kwa upande wa gharama ya mafunzo kwa madereva kwa Sh.560,000 hakikupangwa kabisa katika vikao mbalimbali vilivyo kuwa vikifanyika.

Amesema madereva ambao leseni zao zimekwisha au zitaisha watabadilishiwa /kuhuisha kwa utaratibu wa zamani bila kuulizwa vyeti vya mafunzo mafupi.

Amewataka madereva kuwa wavumilivu kwa matatizo na changamoto zao kwani kamati ya kudumu ya kutatua matatizo katika sekta ya usafirishaji iliyoundwa na Waziri Mkuu itayapatia ufumbuzi wa kudumu.
Kamanda wa Kikosi cha Usalama Barabarani,Naibu Kamishina wa Jeshi la Polisi (DCP),Mohamed Mpinga akizungumza na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam, kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha MaderevaTanzania(CHAMAMATA),Clement Masanja. 
Mwenyekiti wa Chama cha MaderevaTanzania(CHAMAMATA),Clement Masanja akizungumza na waandishi wa habari katika mkutano uliofanyika kwenye ukumbi wa Idara ya habari MAELEZO leo jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad