Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii.
Kampuni ya Majisafi na Majitaka Dar es Salaam(Dawasco)imeanza rasmi operesheni kuwakamata watu waliojiunganishia maji kwa njia haramu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam,Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema operesheni hiyo itafanyika kanda zote za jiji la Dar es Salaam ikiwa ni kutaka jamii kuacha tabia hiyo.
Amesema kuwa wizi wa maji unafanya watu ambao ndio wateja wa Dawasco kukosa maji na kupata watu wasio wateja wakiwa wameunganisha maji kwa kiwango kikubwa.
“Hatuwezi kuacha maji yawe yanaibiwa huku wateja wetu wanaolipia ankara zao wakikosa, ni lazima hatua zichukuliwe kwa wale wote watakaobainika na wizi wa maji yetu”amesema Luhemeja.
Luhemeja amesema kwa wale watakaotoa taarifa za mtu anayeibia Dawasco atapewa Sh.500,000 ambapo kufanya hivyo watamlinda dhidi ya huyo mwizi wa maji.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Dawasco,Mhandisi,Cyprian Luhemeja akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani kuhusiana na operesheni ya wizi wa maji jijini Dar es Salaam.
No comments:
Post a Comment