Meneja Mdhibiti Viwango wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Conchesta Ngaiza (kulia) akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Calvin Martin akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
Meneja wa Kiwanda cha Dar es Salaam cha Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Calvin Martin (kulia) akimuelezea jambo Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
Mshauri
wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) Phocus Lasway akitoa maelezo kwa Naibu
Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe
(kulia) wakati wa ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo
Ilala. Kushoto ni Mkurugenzi wa Usalama na Chakula wa Mamlaka ya
Chakula, Dawa na Vipodozi, Raymond Wisenge. Wizara ilionesha kuridhishwa
na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
Naibu Waziri wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Kebwe Stephen Kebwe (mwenye koti) akiwa katika picha ya pamoja na viongozi mbalimbali a wafanyakazi wa Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) na watumishi wa wizara hiyo baada ya ziara ya Kiwanda cha Dar es Salaam cha TBL kilichopo Ilala. Wizara ilionesha kuridhishwa na viwango vinavyozingatiwa na TBL katika uzalishaji wake.
Wizara
ya Afya na Ustawi wa Jamii imeonesha kuridhishwa na viwango
vinavyozingatiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) katika uzalishaji wa
bia zake.
Kauli hiyo imetolewa na Naibu Waziri wa
Wizara hiyo Dk Kebwe Stephen Kebwe wakati wa ziara ya kiwanda hicho
ikiwa ni sehemu ya utaratibu wa wizara yake kutembelea maeneo yaliyo
katika utaratibu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii.
“Hapa TBL tumegundua kuna uwelewa wa hali ya juu kwa watumishi, wafanyakazi, wasimamizi na menejimenti ya
kampuni hii kwa kweli viwango ni vizuri na hasa katika ufuatiliaji wa
wa afya za wafanyakazi,” alisema na kuongeza kuwa walijionea uzalishaji
wa bia mbalimbali kiwandani hapo kwenye chupa na kadhalika.
Kwa
mujibu wa Naibu Waziri huyo, malengo mwaka huu ni kufanya usimamizi
katika maeneo mbalimbali yanayotoa huduma kwa wananchi kama viwanda na
kuogeza ni lazima viwanda viendane na viwango vinavyotakikana kisheria
na kimataifa na kwamba wizara yake sasa hivi haikai na kusubiri ripoti
za mezani bali wanatembelea maeneo yaliyo chini yao ili kujihakikishia
kuhusu suala la viwango.
Naibu
Waziri huyo, ambaye aliambatana na viongozi mbalimbali kutoka wizarani
na Mamlaka ya Chakula, Dawa na Vipodozi (TFDA), aliwapongeza viongozi wa
TBL kwa kujipanga vizuri katika utendaji wao.
“Tumetembelea
viwanda mbalimbali lakini hapa mmejipanga vizuri zaidi, alisema baada
ya kupokea maelezo mbalimbali kutoka kwa viongozi wa TBL waliokuwepo
kwenye ziara hiyo.
Dk.
Kebwe pia aliipongeza TBL kwa kuwa mstari wa mbele katika kuwajali
wafanyakazi kwa kuanzisha Programu ya Ukimwi katika sehemu ya kazi
ambayo pamoja na mambo mengine inalenga kuhamasisha upimaji wa mara kwa
mara na pia kuhumiza matumizi ya kinga dhidi ya ugonjwa huo.
Katika
maelezo ya utangulizi, Naibu waziri huyo alielezwa kuwa TBL ina
utaratibu wa kupima wafanyakazi wake mara moja kwa mwaka na kwa kipindi
cha kuanzia Aprli mwaka jana hado Machi mwaka huu zaidi ya asilimia 83
ya wafanyakazi walipima afya yao kuona kama wameathirika au la.
“Hii
ni dalili nzuri sana na nawapongeza kwa hatua hii na ni matumaini yangu
kuwa kuanzia sasa na kuendelea mtaanza kupima mara mbili kwa mwaka
nivyo sheria inavyotaka,” alisema.
Meneja
wa Kiwanda Cha Dar es Salaam, Calvin Martin, alisema wamefarajika mno
kwa ujio huo wa Naibu Waziri ili aweze kujionea namna kampuni hiyo
imekuwa ikizingatia suala la viwango katika uzalishaji wake.
“Tumewaonesha
maeneo yote na wameonesha kuridhishwa na viwango na haua ambazo bidhaa
zetu zinapitia kabla ya kwenda kwa mlaji,” alisema na kuongeza kuwa wana
nia ya kuendelea kuboresha viwango vyao ili kampuni hiyo iendelee kuwa
bora zaidi.
No comments:
Post a Comment