HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, April 27, 2015

RAIS KIKWETE AIFARIJI FAMILIA YA MAREHEMU BRIGEDIA JENERALI MSTAAFU HASHIM MBITA LEO

 Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.  Marehemu anatarajiwa kuzikwa siku ya Jumatano katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es salaam baada ya Swala ya Alasiri katika msikito wa Mtoro,  baada ya kupata heshima zote za kijeshi asubuhi yake katika makao makuu ya Jeshi Upanga, Dar es salaam.
  Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiangalia wakati Mama Salma Kikwete akiweka saini katika kitabu cha maombolezo alipokwenda kuifariji familia ya Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015. 
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma kikwete wakimsikiliza mtoto wa Marehemu Bw. Iddi Mbita (shati jeupe) kuhusu taratibu za mazishi walipokwenda kuifariji familia ya  Marehemu Brigedia Jeneral Mstaafu Hashim Mbita Temeke Chang'ombe jijini Dar es salaam jioni ya leo April 27, 2015.  
Rais Kikwete akiondoka msibani akiwa ameongozana na mtoto wa marehemu Bw. Iddi Mbita, Balozi Tambwe, Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Saidi Meck Sadik na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe Sophia Mjema. Picha na IKULU

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad