HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, April 28, 2015

NHIF YAENDELEA KUWAHAMASISHA WANANCHI WA KILWA KUJIUNGA NA CHF

Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani (kulia) akikabidhi baadhi ya mashuka kwa Mwenyekiti wa Kijiji cha Chumo, Khatib Riwanda kwa matumizi ya Zahanati ya Kijiji hicho cha Chumo, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi. Katikati ni Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond.Picha na Othman Michuzi, Lindi.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF),  Rehani Athumani akizungumza na Wakazi wa Kijiji cha Chumo juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.
Meneja wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Lindi, Fortunata Raymond akieleza jambo kwa Wakazi wa Kijiji cha Chumo juu ya umuhimu wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.
Mwakilishi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Mtandao wa Mifuko ya Afya ya Jamiii nchini (TNCHF), Kidani Mhenga akiwapa somo Wakazi wa Kijiji cha Chumo juu ya umuhimu wa wananchi hao kujua taratibu zote zinafanywa katika vituo mbalimbali vya Afya na kuhoji mapato na matumizi ya fedha za Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.
Vijana wa Maigizo kutoka Kundi la Jitihada la Nangurukuru, Salum Lezla na Jenipher Gotadi wakiiza kama wazazi wa mtoto aliepoteza maisha kutokana na kukosa matibabu baada ya kukataa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF, wakati wa muendelezo wa Kampeni yake iliyofanyika leo kwenye Uwanja wa Shule ya Msingi Chumo, Kata ya Chumo, Kilwa Mkoani Lindi.
 
Sehemu ya Wakazi wa Kijiji Chumo, Kata ya Chumo wilayani Kilwa wakifatilia kwa makini shughuli nzima za kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika halmashauri kumi nchi nzima.
Afisa Matekelezo na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Salvatory Okumu akiwaelekeza Wakazi wa Kijiji cha Chumo, sehemu husika ya kwenda kujiunga na huduma ya Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inafanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wakati wa muendelezo wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko huo.

Mratibu wa Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa, Fred Mpodachuma akiongoza zoezi zima la upimaji kwa wakazi wa Kijiji hicho.
Wataalam wa Afya kutoka Hospitali ya Kinyonga Wilaya ya Kilwa wakitoa huduma
Daktari kutoka Hospitali ya Kinyonga Wilaya ya Kilwa akimsikiliza kwa makini mmoja wa wazee wa Kijiji cha Chumo wakati akiwashauri juu ya Afya yao.
Vipimo vikiendelea.
Sehemu ya Wakazi wa Kijiji cha Chumo wakiwa wamehamasika na kuamua kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inayofanywa na Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), wakati wa muendelezo wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasiahaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko huo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad