HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Thursday, March 26, 2015

wakazi eneo la sae jijini Mbeya walia na vibaka wanaojificha kwenye mashamba ya mahindi

Wakazi wa eneo la Sae jijini Mbeya, wamelalamikia uwepo wa mashamba ya zao la mahindi yaliyopo kwenye eneo hilo kwani inadaiwa kuwa yamekuwa ni hifadhi ya vibaka wanaopora watu wanaopita katika njia zilizopo kwenye machamba hayo.

Taarifa za awali zinaeleza kuwa Halmashauri ya Jiji Mbeya walitoa zuio la kuwepo kwa kilimo hicho eneo hilo, lakini watu wameendelea kulima.Hivyo hofu inazidi kutawala kwa wakazi wanaokaa maeneo ya jirani/pembezoni mwa Mashamba hayo.
Haya ndiyo Mashamba ya mahindi ambayo yapo jirani kabisa na Mitambo ya kuzalisha umeme wa Tanesco iliopo Sae Jijini Mbeya,ambapo wakazi wamepata hofu kubwa kutokana na kuwepo kwa mashamba haya.
 Ingawa watoto wanapita hapa lakini ni eneo ambalo ni la hatari sana.
 vijana wengi wacheza Kamari , wahuni na wengine wavuta Bangi wanashinda eneo hili la Sae Nyuma ya Mitambo ya Tanesco.
 Hii njia zamani ilikuwa inapitika kwa Urahisi sana kwa sababu kulikuwa hakuna mashamba ya mahindi kama ilivyo sasa, wakazi wa maeneo haya hawapiti kwa sababu ya hali ya ukabaji hata mchana peupe watu hawapiti.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad