.jpg)
Magari yakiwa yameanza kupima kwenye Mzani mpya na wakisasa wa Vigwaza. Mzani huu unapima gari moja kwa muda wa sekunde 30 tofauti na Mzani wa zamani wa Kibaha uliokuwa unatumia dakika moja na nusu.
Mtendaji
Mkuu wa Wakala wa Barabara nchini TANROADS Eng. Patrick Mfugale
ametangaza kuanza rasmi kwa majaribio ya kupima magari kwenye Mzani wa
Kisasa wa Vigwaza mkoani Pwani ambapo majaribio hayo yataendelea hadi
siku ya tarehe 17/03/2015.
Kwa
mujibu wa Eng. Mfugale, mara baada ya majaribio kukamilika siku hiyo
kituo cha Mzani wa Kibaha katafungwa rasmi na magari yataendelea kupimwa
kwenye kituo kipya cha Vigwaza ambacho kina uwezo wa kupima gari moja
likiwa linatembea kwa muda usiozidi sekunde 30 tofauti na mzani wa
zamani uliokuwa unatumia dakika moja na nusu.
Eng.
Mfugale amewataka madereva kufata taratibu zifuatazo katika Mzani huo
mpya utakaokuwa unapima magari yakiwa kwenye mwendo yani weigh-in-motion
i) Magari yanayotakiwa kupimwa kwa mujibu wa sheria ni yote yanayoanzia
tani tatu na nusu.(3.5) Magari yanatakiwa yaendeshwe kwa kupita upande
unaostahili kisheria yaani hayatakiwi kukanyaga mstari mweupe katika
barabara.
Eng.
Mfugale aliongeza kuwa usipofata utaratibu huu katika Mzani taa
nyekundu mbele ya itawaka na dereva kuelekezwa kwenye mzani mkubwa hata
kama hujazidisha uzito na utatakiwa kulipa tozo la dola za Kimarekani
2000 kuashiria kwamba dereva anakwepa mzani.
Eng.
Mfugale alisema kuwa adhabu hiyo ni kwa mujibu wa sheria ya Usalama
Barabarani namba 30 ya mwaka 1973 na kanuni zake za mwaka 2001 kifungu
namba 6(b) ii) Madereva wanatakiwa wazingatie mwendo wa kilomita 50 kwa
saa iii) Madereva wahakikishe kuwa matairi ya magari yao yanapita juu ya
plates za weigh-in motion na kuachana mita 30 yanapokaribia kupita eneo
la Mzani ili kuondoa usumbufu wakati wa upimaji.
Pia
Eng. Mfugale ametoa angalizo kuwa gari lolote litakalozuia magari
mengine kwenye barabara ya maingilio ya Mzani au kwenye mzani wakati wa
upimaji kutokana na ubovu wa magari hayo yatatozwa faini kiasi cha Tsh.
300,000/= au kifungo kisichopungua mwaka mmoja jela au vyote kwa pamoja
na hiyo ni kwa mujibu wa kifungu 50(1) (f)(g)(h)(i) cha Sheria ya
barabara namba 13 ya mwaka 2007.
Mwisho
Eng. Mfugale amewashauri wamiliki wa magari kuhakikisha kuwa madereva
wao wanakuwa na wasaidizi watakaowasaidia kupeleka nyaraka za gari na
mzigo ili kurekodiwa kwenye ofisi za mzani.
Mzani
wa Vigwaza ni wa kwanza kujengwa nchini na una uwezo wa kuchambua na
kubaini magari Weigh-in- Motion yaliyozidisha uzito huku yakiwa
yanatembea.
Pia
kituo hicho cha Vigwaza kina Mzani mkubwa multi deck wenye uwezo wa
kupima gari lolote kwa mkupuo. Pia barabara za kuingia kwenye mzani
mkubwa zenye urefu wa km 1.8 zimejengwa kwa zege lenye uwezo wa kudumu
kwa miaka 50. Picha na Stori kwa Hisani ya Kitengo cha Mawasiliano
Serikalini GCU-Wizara ya Ujenzi
Mtendaji
Mkuu wa TANROADS Eng. Patrick Mfugale akiwaonyesha Waandishi wa Habari
namna ya upimaji wa magari katika Mzani mpya wa Vigwaza ambao umeanza
kufanya kazi kwa majaribio.
No comments:
Post a Comment