HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, March 24, 2015

JAMANI MSIONE KIMYA KWA KUTOONEKANA KWANGU HUKO MJINI,HUKU USWAZI KWETU HALI BADO NI NGUMU KAMA HIVI

 Homu kwangu ni nyuma ya Kamera iliyopata taswira hii,na hapo mbele ilipo hiyo swimingi puli ndipo ilipo njia ya kuja tauni.hivyo tunasubiri jua liwake ili maji yakauke walau kidogo ndio tutoke.
 Pale mbele ni nyumbani kwa jirani yangu na mshkaji wangu wa kitambo,Bw. Kintinku ambaye kwa sasa salamu tunapeana kwa mbali tu,maana kukutana na mpaka hii swimingi puli ikauke.
 Jirani akiwaza atoke vipi.
 Wakina nanihii ndio hata Msalani hakuendekeki kwa jinsi hali ilivyo.
 Hakutokeki kabisa yaani.
 Jamani huku kwetu hata wageni hawawezi kuja,labda kama wanamaboya ya kuogelea.
Hii ndio staili ya kutembea huku kwetu kwa waliojitoa muhanga kama mdau hapa.
Yakizidi,hivi ndivyo tunavyoyatoa.
 "Sijui nijiongeze tu kwa kuanza kufuga samaki???"  Nawaza tu jamani.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad