WASHINDI wanne wakiwa na marafiki zao wa shindano la Ndovu Golden Experience wametembelea hifadhi ya Selous na kujionea vivutio vya aina mbalimbali ikiwemo wanyama wa nchi kavu na majini, chemchem za maji ya moto,kaburi la Kaptani Selous na vingine vingi.
Washindi hao walipatikana katika Droo zilizokuwa zikichezeshwa mwaka jana ambapo jumla ya washindi wanne walifanikiwa kushinda na kujipatia nafasi ya kutembelea hifadhi hiyo wakiwa na marafiki zao kila mmoja.
Akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam jana, Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt ambao ndio waratibu wa shindano hilo Victoria Kimaro alisema, lengo la kuandaa shindano hilo ni kwa ajili ya kuwapa fursa Watanzania kutembelea hifadhi na kujivunia utalii wao wa ndani.
Alisema, kwa kutambua bia yao ya Ndovu inabebwa na nembo ya mnyama Tembo, wanatumia nafasi hiyo kumlinda mnyama huyo kama kampeini yao inavyosema 'Ndovu Defance', ili kunusuru mauaji yake.
"Utalii ni sekta muhimu sana katika kukuza uchumi wa Tanzania, ila utalii mkubwa unaofanyika hapa Tanzania ni wa wageni wa nje, hivyo basi tunaamini kwa kuendeleza kampeini yetu hii ya Ndovu Golden Experience, iliyokuwa ikiendeshwa kwa kutumia namba za chini ya kizibo ya kuwapa fursa muhimu watanzania kujivunia utalii wao,"alisema Victoria.
Aidha Victoria alisema, washindi walikwenda kutembelea hifadhi hiyo Januari 30 na mwaka jana na kutrejea Februari 2 mwaka huu, huku Ndovu wakigharimia malazi, chakula pamoja na usafiri na kuwataka watanzania ambao hawajabahatika kushiriki, wasisite kushiriki awamu nyingine mwishoni wa mwaka huu kwani program hii ni endelevu.
Victoria aliwataja washindi wote waliopata fursa ya kutembelea hifadhi hiyo kuwa ni Sigfrid Masawe, Samson Marwa, Amandi Agusto pamoja na Mussa ambao watapata fursa ya kwenda na wenza wao kila mmoja.
Nae mmoja wa washindi, Sigfrid Masawe kutoka Arusha alishukuru Kampuni ya Bia Tanzania kupitia bia yake ya Ndovu Special Malt kwa program yake ya Ndovu Golden Experience kwa kuwapa fursa kwenda kutembelea hifadhi ya Selous na kujionea vivutio mbalimbali ambavyo kwa gharama zao binasfi wasingeweza.
Masawe alisema, ‘Tunawaomba Ndovu wasiishie hapa waendelee na programu hii na tunawaomba waongeze idadi ya watu ili watanzania wanufaike na wafahamu umuhimu wa kumlinda mnyama tembo anayebeba nembo na bia ya Ndovu.
Baadhi
ya washindi wa program ya Ndovu Golden Experience iliyokuwa ikiendeshwa
na TBL kupitia bia yake ya Ndovu wakirejea jijini Dar es Salaam mara
baada ya kuzulu katika hifadhi ya Selous kwa siku mbili mwishoni mwa
wiki.
Baadhi
ya washindi wa program ya Ndovu Golden Experience iliyokuwa
ikiendeshwa na TBL kupitia bia yake ya Ndovu wakiwa katika picha ya
pamoja na Meneja wa Kampi ya Lake Manze(katikati) walipokwenda kujionea
vivutio mbalimbali katika mbuga hiyo mwishoni mwa wiki.
Meneja
wa Kambi ya Lake Manze akiwaelekeza jambo washindi wa wa program ya
Ndovu Golden Experience iliyokuwa ikiendeshwa na TBL kupitia bia yake
ya Ndovu walipokwenda kujionea vivutio mbalimbali katika mbuga hiyo
mwishoni mwa wiki.
Baadhi
ya washindi wa program ya Ndovu Golden Experience iliyokuwa ikiendeshwa
na TBL kupitia bia yake ya Ndovu wakiwasili katika mbuga ya Selous
kuzulu kwa kujionea vivutio vya aina mbalimbali mwishoni mwa wiki.

No comments:
Post a Comment