HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Friday, February 6, 2015

SAFARI LAGER YAZINDUA SHINDANO LA UCHOMAJI NYAMA KWA BAR MBALI MBALI NCHINI

Meneja wa bia ya Safari Lager, Edidh Bebwa(kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa masindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 uliofanyika Dar es Salaam leo.Kushoto ni Jaji Mkuu wa mashindano hayo, Manase Mwasha.
Jaji Mkuu wa mashindano Safari Nyama Choma, Manase Mwasha(kushoto) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa masindano ya Safari Nyama Choma kwa mwaka 2015 uliofanyika Dar es Salaam leo.Kulia ni Meneja wa bia ya Safari Lager, Edidh Bebwa.
Meneja wa bia ya Safari Lager, Edidh Bebwa(kulia) akimkabidhi kikombe Jaji wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015 wakati wa uzinduzi uliofanyika Dar es Salaam leo.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua rasmi shindano la uchomaji nyama kwa baa mbalimbali lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2015”.

Shindano hili hufanyika kila mwaka, na kwa mwaka huu linafanyika kwa mara ya nane mfululizo na litashirikisha mikoa ya Mbeya, Mwanza, Arusha, Kilimanjaro na Dar Es Salaam. Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo.

Kwa mwaka huu walaji wa nyama choma watatakiwa kupigia baa zao kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kutumia simu za mkononi kwenda namba 0653-215151. Ujumbe huu utatozwa gharama ya kawaida kwa kutuma ujumbe, hakutakuwa na makato ya ziada kwa mitandao yote ya simu. 


Ujumbe utakaopokea utathibitisha kura yako imepokelewa “Asante kwa kupigia kura Bar unayoiamini kwa kuchoma nyama bomba zaidi mkoani kwako kura yako imepokelewa.Nyamachoma na Safari Lager ndio Baa tano zitakazopata kura nyingi zaidi katika kila mkoa zitachuana kwa kuchoma nyama katika tamasha la wazi litakaloandaliwa katika mikoa yote, washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwamo fedha taslimu.

Zaidi ya shilingi milioni ishirini na sita zitatolewa kama zawadi kwa washindi mwaka huu pamoja na zawadi ya kikombe kwa mshindi wa mkoa atanyakuwa donge nono la shilingi milioni moja na cheti cha ushiriki.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam, meneja wa bia ya Safari Lager Bi.Edith Bebwa alisema kwamba, “Lengo kuu la shindano la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora vya uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma.

Tumezingatia maombi ya washiriki mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji nyama itafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”.

Bi.Edith aliendelea kufafanua kwamba, washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha nyama choma za aina tatu; nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na Kiongozi wa jopo la majaji ambao ni wataalamu maarufu nchini katika tasnia hii, bwana Manase Mwasha alielezea kwamba majaji wataangalia kwa makini sana vigezo mbalimbali katika utayarishaji wa nyama choma. Alitaja baadhi ya vigezo hivyo kwamba ni usafi, vifaa vya kufanyia kazi, joto maalum la uchomaji nyama nk.

Bi. Edith aliendelea kusema kwamba, “Tunaomba bar zote kujitokeza katika semina ya utangulizi tutakayofanya katika mikoa yote inayoshiriki, Katika semina hii tutakumbushana mambo muhimu ya kuzingatia ili kumpa mteja nyama choma bora zaidi, muda wote Bi.Edith alimaliza kwa kusema kwamba, “Safari Lager tutaendelea kujitahidi kuhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora ya nyama choma. Tunawaomba sana washiriki kutumia vizuri elimu na uzoefu wanaopata ili kuongeza ubora wa utayarishaji wa nyama choma kwa wateja wetu.

Mashindano haya ya Safari Lager Nyama Choma yatakosa maana sahihi endapo wachoma nyama watakuwa wanashiriki kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi na kusahau yale yote waliyojifunza hadi mwaka mwingine”.   Shindalo la mwaka huu linaongozwa na kibwagizo…. Safari Lager na Nyama Choma

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad