Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakiwa wamebeba jeneza lenye Mwili wa aliyekuwa DCP Mstaafu wa Jeshi la Polisi Tanzania Mzee Andrew Michael Kumalilwa wakiingia katika nyumba yake iliyopo Tabata Segerea kwaajili ya Misa na ndugu, jamaa na marafiki kutoa heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha katika Nyumba yake ya Milele ambapo Marehemu alizikwa katika nyumba kwake Tabata Segerea.
Baadhi
ya Askari wa Jeshi la Polisi Tanzania wakitoa heshima mbele ya jeneza
lililobeba Mwili wa Marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ambae alikuwa
mstaafu wa jeshi la Polisi kwa ngazi ya DCP
Ndugu
wa marehemu akijadiliana jambo na Mmoja wa Askari wa Jeshi la Polisi
wakati wa Kutoa Heshima za mwisho kabla ya kwenda kuupumzisha mwili wa
Mzee Andrew Kumalilwa ambae alizikwa nyumbani kwake Tabata Segerea
tarehe 14 Februari 2015.
Mwakilishi
kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani na Jeshi la Polisi Tanzania, DCP Simon
Siro akitoa maneno mafupi kabla ya kwenda kuupumzisha Mwili wa marehemu
Mzee Andrew Kumalilwa katika nyumba yake ya Milele. Marehemu Andrew
Kumalilwa alizikwa mnamo tarehe 14 February 2015 huko Nyumbani Kwake
Tabata Segerea.
Jeneza
lenye Mwili wa marehemu Mzee Andrew Michael Kumalilwa ukiwa tayari
kushushwa nyumbani kwake Tabata Segerea ambapo misa ya kumuombea na
kutoa heshima za mwisho zilifanyika kabla ya Kwenda kuupumzisha Mwili
wake katika Nyumba yake ya Milele.
Mtoto wa Kwanza wa Marehemu Andrew Michael Kumalilwa, Patricia Andrew akiwa mwenye huzuni wakati wa msiba wa marehemu Baba yake ambapo marehemu alikuwa mstaafu wa jeshi la Polisi Tanzania akiwa na Cheo cha DCP.
No comments:
Post a Comment