HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, February 16, 2015

BABA YAKE DULLY SYKES AZIKWA JIONI HII KWENYE MAKABURI YA KISUTU,JIJINI DAR

Mwili wa baba wa msanii wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes,Marehemu Ebby Sykes ukiswaliwa nyumbani  kwa kaka wa marehemu maeneo ya Kawe jijini Dar leo mchana.Marehemu Ebby Sykes amezikwa jioni hii kwenye makabiri ya Kisutu.
 Mwili wa Marehemu Ebby Sykes ukipandishwa kwenye gari kwa safari ya kwenda kwenye mazishi,makaburi ya Kisutu jijini Dar jioni hii.
 Msanii wa muziki wa kizazi kipya Dully Sykes akiwa amepanda gari lililobeba mwili wa Marehemu baba yake kwa safari ya kwenda kupumzishwa kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar leo
Baadhi ya wasanii pamoja na ndugu na jamaa waliofika kwenye msiba wa marehemu Ebby Sykse
Baadhi ya waombolezaji wakishiriki mazishi ya msanii mkongwe, Ebby Sykes yaliyofanyika leo kwenye makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
 Waziri Mkuu mstaafu, jaji Joseph Warioba akiweka udongo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Said Meck Sadick akiweka udongo katika kaburi la msanii mkongwe mzee Ebby Sykes.
 Mbunge wa Chalinze, Ridhiwani Kikwete akiweka udongo.
 Mbunge wa Temeke, Abbas Mtemvu akiweka udogo katika kaburi la mzee Ebby Sykes
 Mbunge wa Ilala, Mussa Azan Zungu akiweka udongo katika kaburi la mzee Ebby Sykes.
 Dully Sykes (wa pili kushoto) akiwa ndani ya kaburi la baba yake mzee Ebby Sykes wakati wa mazishi yake.
 Ndugu na jama wakishiriki mazishi.
Umati wa watu ukiwa katika makaburi ya Kisutu jijini Dar es Salaam wakati wa mazishi ya baba yake mzazi ambaye pia ni msanii mkongwe mzee Ebby Sykes.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad