Majira ya saa moja asubuhi katika kituo cha Mandara ikiwa ni siku ya pili ya safari ya Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro maandalizi ya muendelezo wa safari hiyo yanaanza.
|
Balozi wa Tanzania katika falme za nchi za kiarabu,Mbarouk N. Mbarouk akiongoza msafara wa Mabalozi kuelekea kituo cha Horombo.
|
Safari inaendelea.
|
Balozi Adadi Rajab anayeiakilisha Tanzania nchini Zimbabwe na Mauritius akitafakari safari ya kuelekea kituo cha Horombo.
|
Mabalozi Patrick Tsere (Malawi) na Balozi Batilda Burian wakivuta pumzi kwanza kabla ya kuendelea na safari.
|
Balozi Grace Mujuma (Zambia) akiongozana na Balozi Mstaafu na Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB),Balozi Charles Sanga wakienda na mwendo wa Mdogo mdogo.
|
Muongoza watalii mkuu msaidizi wa kampuni ya Zara Tour,Theofiri(mwenye miwani) akiwaongoza mabalozi kuelekea kituo cha Horombo.
|
Mabalozi ,Waandishi pamoja na waongoza watalii wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kutembea kwa umbali mrefu kueleka Horombo.
|
Safari ya kuelekea kituo cha Horombo ikaendelea kwa pamoja bila ya kuacahana.
|
Mahala pengine Mabalozi walilazimika kutumia fimbo maalumu kupanda maeneo ambayo yalkuwa na vipando vikali.
|
Mabalozi ,Shamim Nyanduga( Msumbiji) na Radhia Msuya (Afrika Kusini) walilazimika kupaka mafuta mgando katika nyuso zao ili kuzuia kubabuka na jua.
|
Balozo Tsere akipatiwa huduma ya kwanza ya kuchuwa mguu wake ili aweze kuendelea na safari ,kulia ni balozi Batilida Buriani.
|
Balozi Mwinyi aliamua kupoza koo huku akitafakari safari hiyo.
|
Kila mmoja aliamua kupumzika ili kuvuta nguvu ya kumalizia kipande kilichokuwa kimebakia.
|
Maeneo mengine mabalozi walifanya mazungumzo na wageni waliokuwa wakishuka toka kileleni.
|
Hatimaye Mabalozi wakafika eneo la nusu njia kuelekea Horombo na kupata chakula .
|
Wale waliokuwa wamepungukiwa maji waliongezewa kwa kuwa ndio dawa pekee ili kufanikisha kuwez kupanda Mlima Kilimanjaro.
|
Safari ikaendelea.
|
Hataimaye kituo cha Horombo kikaonekana kwa mbali na mabalozi walitembea na kupumzika hapo.
|
Na Dixon Busagaga wa Globu ya jamii kanda ya kaskazini aliyekuwa katika msafara wa Mabalozi kupanda Mlima Kilimanjaro.
No comments:
Post a Comment