Beki wa timu ya Kijitonyama Veterans, Abdallah Sauko, akijaribu kumiliki mpira wakati wa mchezo wa kirafiki kati yao na Kijitonyama United, uliomalizika hivi punde katika uwanja wa Bora Kijitonyama. Katika mchezo huo timu hizo zilitoka suluhu ya bila kufungana 0-0, ambapo mchezo huo ulikuwa ni maalum kwa ajili ya kuukaribisha mwaka mpya wa 2015 na kuuaga 2014.
Beki wa Veterans, Dastan Luoga (kulia) akiwania mpira na mchezaji wa Kijitonyama United, Idd Seif wakati wa mchezo huo.
Mchezaji wa Kijitonyama United Frank Mnenga (wa pili kulia) akijaribu kumtoka mchezaji wa Kijitonyama Veterans, Hemed Ngwesa, wakati wa mchezo huo.
No comments:
Post a Comment