
Wanafunzi wa Madrasatul Dhuriyatul Islamia kutoka Kisiwani Tumbatu Mkoa wa Kaskazini Unguja wakisoma Qaswida wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein.
Ustadh salum Rashid kutoka Amani Wilaya ya Mjini Unguja akisoma Mlango wa Barzanji(4) wakati wa sherehe za Maulid Matukufu ya kuzaliwa bwana Mtume Muhammad (S.A.W.) zilizofanyika jana katika viwanja vya Maisra Suleiman Mjini Unguja mbele ya mgeni rasmi Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed Shein.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed
Shein na Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi (katikati) Makamo
wa Kwanza wa Rais Maalim Seif Sharif,Kadhi Mkuu wa zanzibar Sheikh
Khamis Haji (kulia) Waziri wa katiba na Sheria Abubakar Khamis Bakary
akifuataiwa na makamo wa Pili wa Rais Alhaj Seif Ali Iddi wakisimaa kwa
pamoja na waislamu wengine na Viongozi wakati wa Kumswalia Bwana Mtume
Muhammad S.A.W.katika sherehe ya Maulid iliyofanyika jana viwanja vya
Maisra Suleiman Mjini Unguja.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk. Ali Mohamed
Shein (kulia) wakati alipojumuika na Mashekhe, Viongozi na Waislamu
mbali mbali katika sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume
Muhmmad S.A.W yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman
Mjini Unguja,(pichani) Mufti Mkuu wa Zanzibar Sheikh Saleh Omar Kabi
akitia ubani kama ishara ya Ufunguzi wa Maulid hayo.
Mke
wa Makamo wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Zakia Bilali
(katikati) akiwa na Wake wa makamo wa Pili wa rais wa Zanzibar Mama Asha
Suleiman Iddi (kushoto) na Mama Pili balozi Seif (kulia) pamoja na Wake
wa Viongozi mbali mbali na wananchi wa kawaida wakijumuika katika
sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W
yaliyofanyika jana katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja
ambapo hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita.
Akina
Mama kutoka mitaa mbali mbali ya Mji wa Unguja na Vitongoji vyake
wakiwa katika viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja palipofanyika
sherehe za Maulidi ya Kuzaliwa kwa Bwana Mtume Muhmmad S.A.W ambapo
hufanyika kila ifikapo mwezi kumi na moja mfunguosita na mgeni rasmi
alikuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Alhaj Dk.
Ali Mohamed Shein.
Wanafunzi
wa Vyuo mbali mbali vya Quran na Waislamu mbali mbali waliohudhuria
katika sherehe za Maulid ya kuzaliwa Bwana Mtume Muhammad S.A.W
zilizofanyika jana katika Viwanja vya Maisara Suleiman Mjini Unguja kama
wanavyoonekanwa Pichani.
Picha na Ikulu.
No comments:
Post a Comment