HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, January 3, 2015

kishalia hapa,tena mchana kweupeeeeee

 Wasamalia wema wakifanya utaratibu wa kumuokoa Dereva wa Gari aina ya Isuzu Trooper iliyopiga mweleka katika makutano ya Shule ya Msingi Oysterbay,mara baada ya kugongana na gari nyingine aina ya Toyota Vitz iliyokuwa ikitokea upande wa Coco Beach jijini Dar mchana wa leo na kupekea dereva wa Gari hii (alikuwa ni Mama mtu mzima ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja) kuumia sehemu ya kiuno na mkono.Gari hii ilikuwa inatokea upande wa St. Peter's kuelekea Morogoro Store na Vitz ilikuwa ikitokea upande wa bahari na kuvuka ghafla barabara hiyo.
 Mashuhuda wakiwa wameizunguka gari hiyo mara baada ya kufanikiwa kumtoa Mama aliekuwa akiendesha Gari hilo.
 Hivi ndivyo ilivyo hii Toyota Vitz baada ya kuhongana na Isuzu Trooper iliyopinduka.
Huyu ndio Mama aliekuwa akiendesha Gari iliyopinduka.Picha na Mdau Pius Micky.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad