Nikiwa mzigoni kuwajibika kama ilivyo kawaida yetu katika maisha,nilipokea simu kutoka wadau wa Kampuni ya Cocacola na kuona kuja kukutana nami,sikusita na niliwakaribisha kazini kwangu.walipofika niona mwanadada huyu aitwae Jacqueline Ngulla na kunikabidhi Box hilo pichani ambalo ndani yake kulikuwa na kinywaji murua kabisa cha CocaCola ambacho upande mmoja kilikuwa kimeandikwa jina langu mimi mwenyeweeeee...... yaani ilikuwa ni bonge la sapraizzzz kutoka CocaCola,kiukweli nimefurahi kwa kuona Kampuni hii ikiutambua mchango wangu katika Jamii. kwa kupitia hashtag hii #ShareaCokeTZ nawapa big up sana CocaCola.
Furaha iliendelea na nikapata nafasi ya kunogesha picha na kina Dada Warembo,Asha Kirambi (shoto) na Jacqueline Ngulla (kulia) walioiwakilisha CocaCola katika kuniletea zawadi yangu hiyo ya Mwaka mpya 2015.
No comments:
Post a Comment