Katika mipindi cha makuzi ya watu wengi enzi hizo, hatua hizi bila shaka wadau wengi wenu mmezipitia huenda zote au moja,libeneke Mtaa kwa Mtaa leo likiwa kitaani limezama na kunasa baadhi ya taswira na kuzimwaga uwanjani hapa kwa ajili ya kukumbushana tu niwapi tulipo toka mpaka leo unaitwa baba,mama kaka au mjomba lakini unakumbuka hatua zile zilizo fanikisha tufike hapa,shuhudia na jikumbushie kupitia libeneke la mtaa kwa mtaa blog.picha na Fadhiri Atick mr pengo.
leo mpaka nihakikishe nina paa kama ndegee.
mhh....hivi vidumu vyote inabidi nipeleke nyumbanii bila hivyo sili leo.
"ngojeni basi nawavunjia wazee mbona hivyoo" mambo ya kukatiana barafu.
nahakikisha leo anatembelea rimu,haiwezekani kila siku atunyime lifti.
dogo tuliaa nikuchimbiee wewe katafute majii bana msumali ni wangu.
aaahaa wewe unanipigaa pichaa,nataka nikafuee nguo za skuu kuu kabisaa
hawaniwezi hawa mi ndo mzee wa shabahaaa.


No comments:
Post a Comment