
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akimkaribisha msanii Naseeb Abdul “Diamond” na kumpongeza kwa kushinda tuzo tano za muziki za kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam siku ya Jumanne Desemba 23, 2014 . Kutokana na sababu zisizoweza kuzuilika, Mshindi wa Big Brother Africa Idris Sultan hakuweza kufika Ikulu kuonana na Rais Kikwete siku hii.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Nassib
Abdul “Diamond” wakati akimuonesha moja ya tuzo kati ya tuzo tano za
muziki za kimataifa alizoshinda mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam
leo Jumanne Desemba 23, 2014. kulia ni Mkurugenzi wa Maendeleo ya
Utamaduni Katika Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Profesa
Hermas Mwansoko.
Rais Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akipata maelezo toka kwa msanii Nassib
Abdul “Diamond” juu ya ushindi wake wa tuzo tano za muziki za
kimataifa mwaka huu, Ikulu jijini Dar es salaam Jumanne Desemba 23,
2014.
No comments:
Post a Comment