HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, December 6, 2014

Mjue Abdul Makuku kijana aliejiari kwa uchinjaji Kuku

Kamera ya Mtaa kwa Mtaa katika katiza katiza zake,iliweza kukutana na mtaalamu wa operesheni za kuku aliejitambulisha kwa jina la Abdul ambaye amekuwa akijizoea sifa kede kede kutoka kwa wateja wake hasa kwa uhodari wake wa kuwaandaa Kuku hao.huyu bwana kazi yake ni kuchinja na kuandaa tu kisha wenye mali wanakuja kuchukua na kwenda kuwafanya vitoweo,Abdul anasema kwa siku anazilaza kuku si chini ya 50.Huyu bwana ameamua kujiajiri kwa kazi hii huku akitoa Rai kwa vijana wengine kuacha kujibweteka na badala yake wajitume kama anavyofanya yeye,kwani wakisubiri kuajiriwa watasubiri sana maana hakuna muda tena wa kuchagua kazi.Je unataka kujua huyu bwana anapatikana wapi????,endelea kufuatilia Libeneke la Mtaa kwa Mtaa kila siku na kila wakati ili uweze kupata Uhondo zaidi.Pichani ni Bw. Abdul akiendelea kuzifanyia upazuaji kuku kede kede huku zingine zikiendelea kusubiria huduma yake.
Bw. Abdul akiwa na timu yake wakiendelea kuzishughulikia kuku vilivyo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad