Meneja wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa(katikati)
akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati wa
kutangaza zawadi za fainali za Kanda za mashindano ya bio za makasia
zijulikanazo kama “Balimi Boat Race” zinazodhaminiwa na bia ya Balimi
Extara Lager zianzotarajiwa kufanyika katika ufukwe wa Mwaloni jijini
Mwanza leo.
Bingwa wa fainali za mashindano ya mbio za makasia Wanaume, chini ya udhamini wa Bia ya
Balimi Extra Lager yajulikanayo kama “Balimi Boat Race 2014” anatarajia kujinyakulia kitita cha
pesa taslimu Shilingi Milioni 2,700,000/=,Kikombe pamoja na medali za dhahabu kwa
wanakikundi hicho.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Bia ya Balimi Exra Lager, Edith Bebwa alisema
fainali hizo zitaanza majira ya saa tatu na asubuhi na kuendelea katika ufukwe wa Mwaloni jijini
Mwanza ambapo jumla ya vikundi 15 vya Wanaume kutoka katika mikoa mitano ya Kanda ya
ziwa vitachuana kumtafuta bingwa wa Kanda kwa mwaka 2014 na vikundi 11 upande wa
Wanawake.
Edith alisema mikoa ya Kanda ya Ziwa inayoshiriki ni Kigoma,Kagera,Mwanza,Musoma na
Kisiwa cha Ukerewe ambacho kinabeba hadhi ya Mkoa.
Mshindi wa pili Wanaume atazawadiwa pesa taslimu Shilingi 2,300,000/=,mshindi wa tatu
Shilingi 1,700,000/= na wa nne 900,000/=.Wakati mshindi wa tano hadi wa kumi watapata
kifuta jasho cha pesa taslimu Shilingi 400,000/= kila kikundi alisema Edihi.
Upande wa wanawake bingwa wa mwaka 2014 ataibuka na kitita cha pesa taslimu Shilingi
2,300,000/=,kikombe na medali za dhahabu kwa wanakikundi wote.Mshindi wa tatu
atazawadiwa Shilingi 1,700,000/=,wa tatu Shilingi 900,000/= na wa nne 700,000/= wakati
mshindi wa 5 hadi wa 10 watazawadiwa kifuta jasho cha pesa taslimu
Shilingi 250,000/= kila kikundi.
Nae Meneja wa Kampuni ya Bia nchini Kanda ya Ziwa, Malaki Sitaki aliwaomba wakazi wa jiji la
Mwanza na vijiji jirani kujitokeza kwa wingi katika ufukwa wa Mwaloni kushuhudia fainali hizo
zenye mvuto wa pekee na mwisho wafahamu nani atachukua ubingwa wa mbio hizo kwa
mwaka 2014.
Meneja matukio wa TBL Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema vikundi vyote vimeshawasili jijini
Mwanza tayari kwa mpambano wa kumpata bingwa wa mwaka huu na maandalizi kwa ujumla
yamesha kamilika hivyo nae aliwaomba watu wajitokeze kushuhudia mbio hizo.
No comments:
Post a Comment