HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, November 12, 2014

ZAIDI YA WANARIADHA ELFU KUMI NA TANO KUSHIRIKI UHURUMARATHON 2014

ZAIDI ya wanariadha 15,000 kutoka ndani na nje wanatarajiwa kuthibitisha kushiriki katika mbio za Uhuru Marathon ambazo zinatarajiwa kufanyika Desemba 7 kwenye viwanja vya Leaders Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Mratibu wa mbio hizo, Innocent Melleck, alisema kuwa maandalizi yako katika hatua za mwisho huku akimtaja Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Mrisho Kikwete, anatarajiwa kuongoa mbio hizo.

Melleck pia alikabidhi ada ya Sh. Milioni mbili kwa Chama cha Raidha Tanzania (RT) na Sh. Milioni moja kwa wenyeji Chama cha Raidha Mkoa wa Dar es Salaam (DAAA), ili kupata kibali cha kuendesha mbio hizo.

Mratibu huyo alisema kuwa fomu kwa ajili ya kushiriki mbio hizo zimeanza kutolewa jana na jijini zinapatikana katika maduka yote ya TSN, huku pia zikitolewa kwenye mikoa ya Arusha, Moshi mkoani Kilimanjaro na Leaders.

“Tunawashukuru wadau wote walioshiriki katika kujiandaa kushiriki mbio hizo hasa klabu za jogging ambazo zinahamasisha wanariadha kushiriki mbio hizo zenye kuhamasisha Amani, ushirikiano na mshikamano,” alisema Melleck.

Katibu Mkuu wa RT, Suleiman Nyambui, alisema kuwa chama kimeialika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani, nchi za Afrika Mashariki na mataifa mengine ambayo yako tayari kushiriki mbio hizo zitakazofanyika sambamba na sherehe za Uhuru wa Tanzania.

Nyambui alisema kuwa wanariadha wamejiandaa kuonyesha vipaji vyao na wanaamini yataendelea kukuza vipaji vyao kulitangaza jina la Tanzania. Naye Mjumbe wa DAAA, Tullo Chambo, alisema kwamba chama kimeshiriki kuanzia hatua ya awali na wanawahakikishia wadau kuwa mbio za mwaka huu zitakuwa na mafanikio. Chambo alisema kuwa wanazipongeza klabu na makundi yote yanayoendelea kujiandaa kushiriki mbio hizo na kila kitu kitafanyika kwa kufuata taratibu za kiufundi.

Melleck alitoa rai kwa makampuni na mashirika pia watu binafsi kujitokeza kwa wingi ili kuweza kudhamini mbio hizi kwani bado nafasi ipo kwa wale wote wenye nia ya kudhamini kwa mwaka huu.

Mbio za Uhurumarathon kwa mwaka huu zinadhaminiwa na Kampuni ya Bia nchini TBL kupitia kinywaji chake Grandmalt,Maji ya Uhui,Azam Tv,Tbc 1,Mwananchi Communications Ltd,Magazeti ya Uhuru,Jambo Leo,Michuzi media,CxC Africa,Kitwe General Traders,Samsung,Cokacola,Tindwa Mediacal Service,Gazeti la TABIBU,Konyagi,na TSN SUPERMARKETS.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck (katikati) akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam leo juu ya maandalizi ya mbio hizo kwa mwaka huu ambapo zinataji kufanyika Desemba 7,2014.Kulia ni Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini,Sulemani Nyambui na kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo
Katibu Mkuu wa Shirikisho la Riadha nchini,Sulemani Nyambui akizungumzia namna mbio hizo zitakavyokuwa ikiwa ni pamoja na njia zitakazokuwa zikitumika kwa washiriki wa mbio ndefu.Kulia ni Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck na kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akionyesha moja ya fomu za kujiunga na mbio hizo wakati akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) jijini Dar Es Salaam leo juu ya maandalizi ya mbio hizo kwa mwaka huu ambazo zinataji kufanyika Desemba 7,2014,huku Mgeni rasmi akitazamiwa kuwa ni Rais Jakaya Mrisho Kikwete huku Zaidi ya wanariadha elfu kumi na tano kukadiriwa kushiriki kwa mara ya kwanza.kushoto ni Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akiendelea kuongea na vyombo vya habari.
Kutoka kwenye Kamera: anaonekana Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo akizungumza machache.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck (katikati) akikabidhi ada ya Sh. Milioni mbili kwa Katibu Mkuu wa Chama cha Raidha Tanzania (RT),Suleiman Nyambui (kulia) huku Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo akizungumza machache akishuhudia.
Mratibu wa mbio za Uhuru Marathon 2014,Innocent Melleck akikabidhi ada ya Sh. Milioni moja kwa Mjumbe wa Chama cha Riadha mkoa wa Dar es Salaam,Tullo Chambo.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad