HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Saturday, November 29, 2014

Wadau wakutanapo mambo huwa hivi

Leo nipo Mjini Dodoma hapa (sio kwenye mambo ya Escrow lakini...... teh teh teh....maana naona mshaanza kuguna) nimekuja kwa mambo mengine kabisa nikiambatana na mpiganaji mwenzangu Cathbert Kajuna (Kajunason Blog) (shoto),sasa katika pita pita zetu katika mitaa mbali mbali ya mji huu si ndio tukaingia hapa ndani,mara tunakutana na Mdau Mkongwe kwenye maswala ya Libeneke hapa nchini (ambaye sasa kahamia kabisa huko nchini Italia,ila kaja nchini kwa vekesheni tu),Bw. Baraka Chibiriti (katikati).kiukweli ilikuwa ni furaha sana kukutana na huyu jamaa kwa maana ni mmoja wa watu waliofanikiwa kuwa maarufu sana kupitia Globu ya Jamii ya Ankal Issa Michuzi.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad