UZINDUZI wa filamu ya Wape Salamu Zao unatarajia kufanyika siku ya Jumapili tarehe 9 November katika ukumbi Travetine Magomeni, uzinduzi huo utambatana na ujio wa sesson 2 kipindi cha Ulimwenguni wa filamu cha TBC 1,kinachoongozwa na Juma Mtetwa katika, kivutio kikubwa ni Jackson Kabirigi ‘Kisate’.
“Nimepanga kuacha historia katika uzinduzi wa filamu ya Wape Salamu Zao, kuna vitu vingi sana ambavyo sijawahi kuwaonyesha watazamaji hajawahi kuviona kutoka kwangu tarajieni maajabu,”anasema Kabirigi.
Uzinduzi huu unasindikizwa na gwiji la muziki wa Taarab Bongo mfalme Mzee Yusuf, ambaye naye ameahidi kufanya show ya kipekee haijawahi kutokea hivi karibuni, na kuimba nyimbo zinazotamba na kufanya vizuri Tanzania.
Wasanii nyota wa filamu kutoka Bongo movie watakuwepo wakiwa wamependeza huku zuria jekundu likipamba sehemu ambayo watu watapata nafasi ya kupiga piga katika mapozi, show hiyo ya kufunga mwaka kiingilio ni 8,000/ tu kwa mtu mmoja si ya kukosa.
No comments:
Post a Comment