HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 24, 2014

MSHINDI WA KWANZA WA SIMTANK AKABIDHIWA RAV 4

Kampuni ya Silafrica Tanzania Ltd, inayoongoza kwa kutengeneza vifaa vya plastiki imekabidhi gari aina ya RAV 4 kwa wakala wake wa bidhaa za SIMTANK ambaye aliibuka  mshindi wa kwanza wa shindano la Uza na Ushinde lililokuwa likiendeshwa na kampuni hiyo kwa lengo la kuhamasisha mauzo ya SIMTANK pamoja na kuthamini mchango wa mawakala katika kampuni hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari wakati wa makabidhiano hayo, Ofsa Mkuu wa Mauzo na Masoko wa SILAFRICA, bwana Alpesh Patel alimtangaza bwana Hiren Chandarana kutoka  RAVI STEEL kuwa ndiye mshindi wa kwanza wa promosheni yao.

‘Leo tunamkabidhi zawadi yake mshnindi wa kwanza, ambayo kimsingi inahitimisha promosheni yetu kwa mwaka huu, hivyo niwapongeze mawakala wote walioshiriki promosheni yetu, na wajiandae kujitokeza kwa wingi mwakani’ alisema Alpesh.

Akiielezea zaidi promosheni ya Uza na Ushinde, Bwana Alpesh alisema zaidi ya mawakala 27 wamejishindia zawadi kutoka SIMTANK.

Bwana Alpesh pia alimshukuru bwana Hiren kwa juhudi zake katika mauzo na kuwaomba mawakala wengine kuongeza bidii ili kujiweka katika nafsi kushinda zawadi kutoka SIMTANK siku zijazo.

Akipokea zawadi hiyo Bwana Hiren aliipongeza kampuni ya SIMTANK kwa kuzalisha bidhaa bora ambazo pamoja na kumuingizia kipato lakini zinasaidia watanzania kupata huduma bora.

Naishukuru sana SIMTANK kwa zawadi hii,lakini pia niwape shukrani mawakala wenzangu kwa kushiriki katika kuhakikisha tunaboresha maisha ya mamilioni ya watanzania wanaotumia huduma za maji safi na salama yaliyohifadhiwa katika tanki imara na salama” alisema Hiren.
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya SILAFRICA Tanzania, Alpesh Patel (kulia), akikabidhi funguo za gari kwa mshindi wa shindano la Uza na Ushinde bidhaa za SIMTANK bwana Hiren Chandarani ambaye ni Mkurugenzi wa RAVI STEEL, anayeshuhudia (katikati), Mkurugenzi Mtendaji wa RAVI STEEL, Ravi Chandarana.makabidhiano hayo yalifanyika makao makuuu ya SILAFRICA Tanzania Novemba 22, 2014 jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Mauzo na Masoko wa kampuni ya SILAFRICA Tanzania, Alpesh Patel akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumkabidhi mshindi gari.
Wakiwa kwenye picha ya pamoja.PICHA NA PHILEMON SOLOMON

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad