Mafunzo ya elimu na ujasiriamali kwa washiriki wa shindano la Mashujaa wa
Kesho yanayoratibiwa na kampuni ya Statoil Tanzania, yenye lengo la
kumjenga
kijana kuwa mjasiriamali yamekamilika hivi karibuni.
Akibainisha aina ya mafunzo ya ujasiriamali waliyopata vijana hao, Erick
Mchome Afisa Mahusiano wa Statoil-Tanzania amesema kuwa
Mafunzo waliyopata vijana hao yamelenga kuwawezesha vijana kuandika
mpango wa biashara ikiwa ni hatua ya awali katika harakati za ujasiriamali.
Pamoja na hilo vijana pia wamefundishwa kujenga uwezo wa kujieleza kwani
sifa moja ya mjasiriamali ni kujiamini na kuweza kusimama mbele ya wateja
kunadi biashara yake.
‘’ Tumekuwa na siku nne nzuri za mafunzo na ni imani yetu kuwa vijana hawa
hamsini na ziaidi watakuwa chachu ya mafanikio kwa vijana wenzao kwani
mafunzo haya yamewatoa kutoka sehemu moja kwenda sehemu nyingine,’’
alisema Mchome.
Sambamba na hayo vijana hao ambao walifikia idadi ya hamsini na zaidi
wamefundishwa namna ya kujijenga kama wajasiriamali ikiwa ni pamoja na
namna za kutafuta mtaji, kupanga mapato na matumizi na pia kutenga faida
kwa kila biashara watakayofanya.
Lengo la mfunzo haya ni kuchochea ari ya ujasiriamali kwa vijana ambao
wameshiriki na kuingia awamu ya pili ya shindano la mashujaa wa kesho. .
Kwa upande vijana waliochaguliwa kuingia hii awamu ya pili wao wamesema
kuwa elimu waliyoipata imewafungua macho na kupanua mawazo sana.
Majadiliano yamewaonyesha wazi kwamba kuna fursa nyingi sana nje ya
kuajiriwa.
“Nawashukuru Statoil-Tanzania pamoja na wasimamizi wa mafunzo haya
kwani
elimu tuliyopata hapa ni msingi mkubwa kwa sisi kuwa wajasiriamali, kufanya
biashara zetu ilitukamate fursa za biashara ambazo zipo mbele yetu. Kuna
njia
nyingi sana za kutafuta maisha ”, Alisema Ally Seleman mshiriki wa shindano
la
Mashujaa wa Kesho.
Mafunzo ya elimu ya biashara na ujasiriamli yalianza toka tarehe 27 Oktoba
2014 na kuendelea kwa siku nne.
Mara baada ya mafunzo hayo kukamilika vijana
wamepewa siku 12 za kuaandika mawazo ya biashara na kuyakusanya siku
ya
jumatano ya tarehe 12 mwezi Novemba ili kuweza kuingia katika awamu ya
pili ya mchakato wa kupata washindi wa shindano hili la Mashujaa wa kesho.
Shindano la mashujaa wa kesho lilizinduliwa mnamo mapema mwezi
Septemba na linatarajiwa kufika kilele mwanzoni mwa mwezi Desemba
ambapo mshindi atajinyakulia kitita cha dola za kimarekani elfu tano kutoka
kampuni ya Statoil.


No comments:
Post a Comment