HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, November 3, 2014

BOA Tanzania yakabidhi zawadi mbali mbali kwa washindi wake leo

Meneja Mwanandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa BOA Tanzania, Bw. Solomon Haule  akizungymza na waandishi wa habari (hawapi pichani) kuhusu kampeni ya benki ya ufunguzi wa akaunti mpya,ambayo inawawezesha wateja wake watano kujinyakulia zawadi mbali mbali.
Mteja wa Benki ya BOA aliejishindia zawadi ya simu aina ya Samsung Galaxy Grand Duos,Ibrahim Agwanda akiionyesha simu hiyo kwa wanahabari (hawapo pichani) mara baada ya kukabidhiwa na Meneja Mwandamizi wa Fedha wa BOA, Bw. Cleopa Dickson.

Benki ya Afrika Nchini Tanzania (BOA Tanzania) imewatunukia wateja watano wenye bahati ya pekee zawadi  za aina mbalimbali kwenye kampeni yake inayoendelea kuhusu ufunguzi wa akaunti mpya na kuendelea kuweka akiba katika zabuni yake mpya ili kuhimiza tabia ya kujiwekea akiba ncini.

Meneja Mwanandamizi wa Masoko na Mawasiliano wa BOA Tanzania, Bw. Solomon Haule alipokuwa anaongea kwenye sherehe fupi ya kuwatunuku tuzo washindi mwishoni mwa juma kwenye makao makuu ya Benki jijini Dar es Salaam alisema kwamba wateja wapya na wa zamani wa Benki wote bado wana nafasi kubwa ya kushinda tuzo mbalimbali za papo kwa papo wakifungua akaunti mpya au wakiweka fedha kwenye akaunti zao.

“Tuna furaha kubwa kwamba baada ya kuchezesha bahati nasibu kwa mwezi Oktoba, 2014 washindi wenye bahati ya pekee wamejishindia vitu mbalimbali vifuatavyo: pikipiki, tuzo ya fedha taslimu, vocha 100,000 za kununulia zawadi mbalimbali, simu za aina ya Samsung Tablet na Samsung Galaxy Grand,” alisema.

Bw. Haule aliwataja washindi kuwa ni Tom Gathari (pikipiki), John Raphael (simu aina ya Samsung Tablet), Ibrahim Agwanda (simu aina ya Samsung Galaxy Grand Duos), Mary Mushi (tuzo ya fedha taslimu Tshs. 500, 000) na mshindi wa mwisho kuwa ni Innocent Msigwa ambaye alijishindia vocha za kununulia zawadi mbalimbali zenye thamani ya Tshs.100, 000.

Bw. Haule aliongeza kwamba wateja watajishindia tuzo za papo kwa papo kama vile miavuli ya mvua, vishikizi vya funguo, majaa makubwa, jezi, simu aina ya Nokia, na kuwa bahati nasibu itakuwa ikichezeshwa kila mwezi ambapo kutakuwa na washindi ambao watapata simu aina ya tablet, pikipiki na mafuta, simu aina ya Samsung smart pamoja na vocha.

Meneja Mwandamizi wa Fedha wa Benki hiyo, Bw. Cleopa Dickson akifafanua mchakato wa kampeni inayoendelea alisema: “wateja ambao wanafungua akaunti kwa salio la chini linalotakiwa watafuzu kuingizwa kwenye bahati nasibu na wanaweza kujishindia tuzo mbalimbali za papo kwa papo mara moja.” Kisha aliongeza kwamba wale ambao wataweka akiba kwenye akaunti zao za kudumu pia watakuwa na nafasi ya kujishindia riba yenye thamani ya hadi asilimia 10.

Kampeni ya‘weka akiba ushinde’ ambayo ilizinduliwa mwezi Septemba, 2014 ilitarajiwa kuendelea hadi mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu na mshindi wa jumla ana nafasi ya kujishindia gari jipya kabisa aina ya Toyota Brevis.

 “Kampeni pia inakusudia kukuza utamaduni wa kujiwekea akiba miongoni mwa Watanzania kwa kujumuisha tuzo za kifedha kwa kuwapatia tuzo wateja ambao wanafungua akaunti mpya pamoja na Benki yetu,” alisema  Meneja Mwanandamizi wa Masoko na Mawasiliano.

Kwa upande wake, mmoja wa washindi, Bw. Ibrahim Agwanda, aliishukuru Benki kwa kumthamini kuwa mmojawapo wa wateja wake waaminifu kwa kumzawadia tuzo kubwa na kuzitaka taasisi nyingine za kifedha kuiga mfano wa Benki ya BOA Tanzania wa kuwajumuisha watu kwenye masuala ya fedha.

Kampeni ya ‘weka akiba ushinde’ inaendeshwa kwenye matawi yote ya Benki nchini Tanzania.  Benki ina matawi 10 jijini Dar es Salaam, matawi mengine yapo mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Morogoro, Mwanza, na Mtwara pamoja na maeneo ya Mtibwa, Tunduma na Kahama. Nchini Tanzania, Benki imekuwa ikitoa huduma kwa zaidi ya miaka 8 kwa makampuni makubwa na biashara ndogo na za kati.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad