Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo, akimpa maelezo ya ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mkuu wa Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi Susan Omari alipotembelea mradi huo ulioko eneo la Isikizya Wilayani Uyui jana. (Picha kwa hisani ya Kitengo cha Mawasiliano ya Umma na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
Mwonekanao wa nyumba za gharama nafuu zilizojengwa na NHC eneo la Isikizya Mkoani Tabora.
Nyumba 38 zilizojengwa karibu kabisa na Makao Makuu ya Wilaya ya Uyui eneo la Isikizya. Nyumba zingine 12 zimejengwa upande wa pili wa barabara eneo la Isikizya.
Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Chilambo akitoa maelezo kwa Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii Bi. Susan Omari yanayohusu viwanja vya Shirika vilivyoko eneo la Itetemia Manispaa ya Tabora.
Meneja wa Mkoa wa Tabora Bw. Erasto Chilambo akielezea hatua mbalimbali zilifikiwa na Mkoa huo za kutengeneza nyumba za Shirika. Hili ni mojawapo ya jengo la Hoteli ya Golden Eagle baada ya kufanyiwa matengenezo.
Sehemu ya Maafisa Vijana wakisikiliza mada iliyotolewa na Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari (hayuko pichani) alipoelezea mpango wa NHC wa kugawa mashine kwa ajili ya kusaidia vijana kwenye Halmashauri zote za Wilaya hapa nchini. Jumla ya mashine 656 zimeshambazwa kwa ajili hiyo.
Washiriki wa semina iliyotolewa na NHC wakisikiliza mada kwa makini
Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano na Huduma kwa Jamii wa NHC, Bi Susan Omari akitoa mada juu ya mpango wa NHC wa kusaidia vijana mashine za kufyatulia matofali katika Halmashauri zote za Wilayanchini.
No comments:
Post a Comment