Zoezi la Ushirikiano Imara linalojumuisha nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki
limefunguliwa leo nchini Burundi na Makamu wa Kwanza wa Rais wa chi
hiyo. Gwaride maalumu linalojumuisha majeshi yote ya nchi wanachama
lilikuwa limesimama mbele ya wageni mbalimbali katika uwanja wa kambi
ya kijeshi ya Muzinga nje ya mji wa Bujumbura wakati Makamu huyo wa
Kwanza wa Rais alipokabidhi Bendera ya jumuiya kuashiria kuanza rasmi wa
mazoezi hayo.
Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) liliwakilishwa na Meja
Jenerali James Mwakibolwa ambaye ni Mkuu wa Mafunzo na Utendaji Kivita
Makao Makuu ya Jeshi.
Mazoezi haya ya medani hufanyika kila mwaka katika moja ya nchi
wanachama kwa utaratibu wa kupokezana yakiwa na lengo kuu la kudumisha
ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama.
Pamoja na mambo mengine, mazoezi haya yatatoa fursa kwa nchi
wanachama kuandaa na kuweka mikakati ya pamoja katika kukabiliana
na matishio mbalimbali yanayoweza kutokea katika ukanda wetu wa afrika
mashariki.
Maudhui makuu ya zoezi la mwaka huu yanajikita katika kukabiliana na
changamoto katika ulinzi wa amani, majanga ya asili na ya kibinadamu,
ugaidi, pamoja na uharamia ambavyo vimekuwa tishio katika maeneo mengi
duniani.
Aidha, kutakuwa na mazoezi ya kuyaweka tayari majeshi yetu katika
kukabiliana na magonjwa ya mlipuko ili kupunguza na kuzuia kabisa madhara
ya magonjwa hayo.
kwa ujumla, mazoezi haya ni kipimo cha jinsi gani nchi yetu imejiandaa na
kujiweka tayari kupambana na changamoto hizi kwa mujibu wa taratibu
zilizowekwa na jumuiya.
JWTZ limejiadaa vyema katika ushiriki likishirikisha waajeshi wa fai malimali
ili kutimiza malengo ya nchi yetu na jumuiya kwa ujumla katika kukabiliana na
changamoto zilizotajwa.
Aidha, kikosi cha Tanzania kupitia kitengo cha Uhusiano na Raia (Civil
Military Cooperation) kimepanga kutoa misaada mbalimbali kwa wananchi
wa Burundi waishio maeneo ya karibu na kambi ikiwa ni pamoja na vifaa kwa
ajili ya wanafunzi. Ikumbukwe kuwa, jeshi bora ni lile ambalo askari wake
wamefunzwa vizuri na kupata mzoezi ya mara kwa mara katika kutimiza
majukumu yao, mazoezi ndiyo hulifaya jeshi letu kuwa tayari wakati wote
kuwatumikia wananchi.
Brigedia Jenerali Joseph Chengelela (kushoto)akimkabidhi bendera ya Afrika Mashariki msaidizi wa zoezi mara baada ya kukabidhiwa kutoka kwa mgeni rasmi hayupo pichani siku ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.
Meja Jenerali James Mwakibolwa wa nne kulia akiwa na Brigedia Jenerali Joseph Chengelela wa tano kulia na Mwambata wa JWTZ nchini Burundi kanali Venant Mutashobya wa tatu kulia mara baada ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI.
Picha ya Pamoja ya maofisa wa serikali ya Burundi na Maafisa Wakuu wa Majeshi ya Jumuiya ya Afrika Mashariki baada ya ufunguzi wa zoezi USHIRIKIANO IMARA 2014-BURUNDI
No comments:
Post a Comment