HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, October 26, 2014

MAKAMU WA RAIS MGENI RASMI KWENYE MADHIMISHO YA SIKU YA MSANII KATIKA UKUMBI WA MLIMANI CITY,JIJINI DAR

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tunzo Edward Said Tingatinga msanii aliyejitolea maisha yake kwa Jamii, kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi tunzo Josephat Kanuti msanii aliyejitolea maisha yake katika tasnia ya sanaa Nchini, kwenye maadhimisho ya siku ya Msanii yaliyofanyika jana usiku Octoba 25-2014 katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es salaam.
Wasanii wa ngoma kutoka Ukerewe wakitoa burudani kwenye maadhimisho hayo.
Msanii wa tasnia ya taarab Isha Mashauzi na kikundi chake nao walikuwepo kwenye maadhimisho ya siku ya msanii Mlimani City.

Wasanii wa kikundi cha sarakasi nao walionesha umahiri wao kwenye usiku wa maadhimisho hayo.
Msanii Daimond na kikosi chake wakifanya vitu vyao kwenye maadhimisho hayo.
Wasanii na wananchi mbalimbali waliohudhuria kwenye maadhimisho hayo wakifuatilia kwa karibu matukio mbalimbali yaliyokuwa yakifanyika kwenye ukumbi huo. (Picha na OMR)

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad