Mzee Ally Chikolo akipata huduma ya upimaji wa kiwango cha sukari (rbg) kutoka kwa mtaalamu wa maabara Dkt Mwampale,ambapo upimaji wa afya kwa magonjwa yasiyoambukiza ulikuwa ukitolewa bure na mfuko wa taifa wa bima ya afya sanjari na elimu ya kujiunga na mfuko wa afya wa jamii,katika kata ya nyangamara halmashauri ya lindi vijijini.
Kushoto mwananchi wa kata ya Nangaru,Asha Mtimbwele akijiunga na CHF papo kwa papo baada ya kuhamasika na kuamua kuuza kuku kwa shs 10,000.ili apate huduma kwa mwaka baada ya kugundulika kuwa na shinikizo la damu ( BP) na kisukari.kushoto ni Mratibu wa CHF wilaya ya Lindi vijijini,Goodluck Khatibu akimfanyia usajili na kupatiwa vitambulisho.
wananchi wa kata ya nyangamara wakiwa kwenye foleni wakielekea kupata huduma ya upimaji wa afya baada ya kupewa elimu ya kujiunga na chf.nhif ofisi ya mkoa wa lindi unatekeleza mpango wa elimu kwa umma kwa kuyafikia makundi mbalimbali ya wananchi ili kuhakikisha azma ya kuwafikia wananchi wote wanachangia matibabu kwa asilimia 30% ifikapo juni 2015 inafikwa.
Meneja wa NHIF mkoa wa Lindi,Bi. Fortunata Raymond (mwenye miwani kulia) ,akiendelea kutoa ufafanuzi kwa wananchi kuhusu faida za kuchangia huduma za matibabu kabla chini ya mfuko wa afya ya jamii,kushoto ni salum kazikazi mwananchi wa kata ya nyangamara lindi vijijini.
Afisa Uanachama wa wa NHIF,Margreth Jacka akiwapa elimu ya mfuko wa afya ya jamii sambamba na NHIF kwa wananchi na wanachama waliojitokeza kupima afya na elimu.
No comments:
Post a Comment