HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Tuesday, September 2, 2014

MH. BENDERA AFUNGUA WARSHA YA SIKU MBILI YA WAANDISHI WA HABARI INAYOHUSU UMUHIMU WA UTOAJI TAARIFA ZA HALI YA HEWA KWA UMMA,MKOANI MOROGORO LEO

JAMII nchini imepewa wito wa kuacha kudharau taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na Mamlaka ya hali ya hewa nchini ili kupunguza uwezekano wa kutokea majanga makubwa.

Wito huo umetolewa leo na Mkuu wa mkoa wa Morogoro, Joel Bendera, wakati akifungua warsha ya siku mbili kwa wanahabari iliyoandaliwa na Mamlaka ya Hali hewa nchini (TMA).

Bendera ametoa wito huo siku mbili kabla ya TMA kutoa utabili wake wa hali ya hewa wa msimu wa Oktoba mpaka Desemba mwaka huu. Bendera alisema kuwa TMA imekuwa mstari wa mbele kutoa taarifa za hali ya hewa pamoja na tahadhari zake lakini wananchi walio wengi wamekuwa wakidharau tahadhari zinazotolewa na Mamlaka hiyo.

“Kama wananchi watakuwa wakifanyia kazi tahadhari zinazotolewa na TMA, itasaidia kupunguza madhara yanayotokana na mabadiliko ya hali ya hewa.., Serikali inapata tabu kuwasaidia wananchi yanapotokea majanga.., lakini ukiangalia kabla ya majanga kutokea TMA wanakuwa tayari wameshatoa tahadhari ila sisi wananchi tuzidharau taarifa zao” alisema Bendera.

Aidha, alisema kuwa majanga ya hasili ni ngumu kuyaepuka lakini kupitia tahadhari za TMA inawezekana kupunguza madhara ya majanga hayo.

Kwa upande wake, akimkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa TMA, Dkt Agness Kijazi, alisema kuwa Mamlaka yake inatambua umuhimu wa wanahabari katika kufikisha taarifa za hali ya hewa kwa wananchi na ndio sababu ya kuwapa elimu itakayosaidia kuwaelimisha wananchi juu ya taarifa za hali ya hewa zinazotolewa na mamlaka hiyo.

Katika hatua nyingine, Mamlaka hiyo mjini hapa kesho inatarajia kutoa utabiri wake wa mvua kwa msimu huu wa kuanzia Oktoba mpaka Desemba.
 Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera akitoa hotuba yake ya ufunguzi wa Warsha ya siku mbili ya Waandishi wa Habari ilinayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma,inayofanyika kwenye hoteli ya Oasis mjini Morogoro.Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi na kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya Wanahabari inayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma wakisikiliza kwa makini hotuba ya ufunguzi wa warsha hiyo iliyokuwa ikisomwa na Mkuu wa Mkoa wa Morogoro,Mh. Joel Bendera.
 Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa akizungumza machache wakati akitoa shukrani kwa mgeni rasmi na kwa washiriki wa warsha hiyo inayoendelea kufanyika hivi sasa kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Oasis,Mkoani Morogoro.
  Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa akizungumza jambo wakati akichangia moja ya mada zinazoendelea kuwasilishwa kwenye warsha hiyo inayoendelea hivi sasa kwenye ukumbi wa mikutano wa hoteli ya Oasis,Mkoani Morogoro.
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi akisisitiza jambo wakati akijubu moja ya maswali yaliyoulizwa na waandishi wa habari wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya Wanahabari inayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,inayohusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma
Muwasilishaji wa Mada ya kwanza katika warsha hiyo,Bi. Mecklina Merchades akiwasilisha mada iliyohusu Utekelezaji wa programu ya utoaji huduma ya hali ya hewa duniani.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Agness Kijazi na Mkurugenzi wa Huduma za Utabiri wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini,Dkt. Hamza Kabelwa wakisikiliza kwa makini uwasilishwaji wa mada mbali mbali zinazoendelea kuwasilishwa kwenye warsha hiyo.
 Baadhi ya Waandishi wa Habari wanaoshiriki kwenye Warsha ya siku mbili ya Wanahabari inayoendeshwa na Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini kuhusu umuhimu wa huduma za hali ya hewa,ushirikishwaji na usambazaji wa taarifa za hali ya hewa kwa umma wakifatilia kwa makini mada zinazoendelea kutolewa kwenye warsha hiyo.
 Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad