HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Sunday, July 20, 2014

WADAU TUJIHADHALI NA WATU HAWA WANAOSEMA WANATOKA TANESCO KUMBE NI VISHOKA

leo asubuhi wamekuja watu 6 nyumbani wakasema wanatoka tanesco wamekuja kucheki mita ya luku.

wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye gps yao kuwa umeme hauendi vema.

Macho yakatutoka,wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia.

nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi?si ingepaswa tulipe kidogo?wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba umeme) huwa kinafyatuka halaf umeme unakwenda zaidi!

 wakakata umeme wakaondoka,tujipange.tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halaf wanalazimisha mambo,wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki.tukapiga simu tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuite polisi.

basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie umeme,mengine j3. wakaja fasta2 wakarudisha umeme.nikawaambia naenda atm wasubiri.nikawaacha na mzee.nikatoka mbio mpaka polisi chuo nikawahadithia wakanipa polisi 3 nikaja nao home,tukawakuta wameondoka.

mzee akawapigia simu waje hela imepatikana.wakasema tukutane mlimani city,tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia.tumemuacha selo,tukaandikisha maelezo.tunasubiri hatua itakayofuata.hiyo picha ndo huyo tuliyemkamata!

Mdau aliekutwa na Mkasa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad