Waziri Mkuu,Mh. Mizengo Pinda akiwa katika picha na Bw. Anic
Kashasha, Mwenyekiti Mtendaji wa TACIN alipomtembelea nyumbani kwake
Oyserbay, Dar es Salaam, jana Jumapili, tarehe 30 Julai, 2014 kumpa taarifa ya
maendeleo ya maandalizi ya Mtwara Festival, itakayofanyika tarehe 16 - 17
Agosti, 2014 katika viwanja vya Chuo Cha Ualimu Mtwara(TTC). Mh. Mizengo Pinda,
atakuwa Mgeni Rasmi wa Mtwara Festival, ambao ni mpango mkakati wa mawasiliano
wa kuhamasisha wananchi wa mikoa ya Mtwara na Lindi, kizitambua fursa
shirikishi zinazosisimuliwa na uchumi wa gesi asilia. Kauli mbiu ya Mtwara
Festival ni "FURSA ZIMEFUNGUKA, TUZITAMBUE, TUJIANDAE,
TUZICHANGAMKIE". Akizungumza mara baada ya kukutana na Waziri Mkuu, Bw.
Kashasha alisema mpango huo wa elimu kwa umma, utachangia kwa kiasi kikubwa
kutengeneza ajira na kipato kwa wananchi wa mikoa hiyo na hivyo kubadilisha
hali za maisha ya wananchi hao.
Thursday, July 31, 2014

Home
Unlabelled
Mh. Pinda Mgeni Rasmi Mtwara Festival 2014
Mh. Pinda Mgeni Rasmi Mtwara Festival 2014
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment