HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Monday, July 21, 2014

MAMIA YA WANANCHI SOMANGA KILWA WAJITOKEZA KUPIMA AFYA BURE,KAYA 70 ZAJIUNGA NA CHF PAPO KWA PAPO WAKIPOKEA MWENGE WA UHURU

Kiongozi wa mwenge kitaifa mwaka 2014,Rachel Kassanda akiwataka wananchi wa kilwa kujiunga na CHF,kwani ndiyo mkombozi wa matibabu sasa kwa kuzingatia maboresho ya huduma za afya yanavyowezekana chini ya sera ya urasimishaji wa majukumu kwa jamii hususani ya uchangiaji baina ya wananchi na serikali,ambapo mfuko wa taifa wa bima ya afya unasimamia mfuko wa afya ya jamii kwa niaba ya serikali ,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe.Abdalla Ulega ambaye ndiye mwenyeji wa mapokezi ya mwenge wa uhuru.
Meneja wa mfuko wa taifa wa bima ya afya mkoa wa Lindi,Fortunata Kullaya akitoa taarifa ya utekelezaji wa zoezi la upimaji afya na mwitikio wa wananchi wa kilwa ambapo takribani wananchi 257 walijitokeza kupimwa afya na kaya 73 zilijiunga papo kwa papo na CHF Kwenye banda la mfuko kwa kiongozi wa mwenge kitaifa kwa mwaka 2014 Rachel Kassanda,ambaye alikagua shughuli mbalimbali zilizokuwa zikitekelezwa kwenye viwanja vya shule ya msingi somanga ambapo mwenge wa uhuru ulipokelewa,kulia ni mkuu wa wilaya ya Kilwa mhe. Abdallah Ulega.
Mkazi wa kata ya somanga Fatuma Likondwe akipata huduma ya upimaji wa shinikizo la damu kutoka kwa daktari Salama Bimbire,zaidi ya watu 257 waliweza kupatiwa huduma za vipimo kwa magonjwa yasiyoambukiza na wastani wa asilimia 58% ya waliopimwa walikutwa na shinikizo la damu (BP) na hawakujitambua hapo kabla.
Wananchi wa Kilwa wakiwa kwenye foleni ya kupata huduma za vipimo kwenye banda la Mfuko wa taifa wa bima ya afya ambapo huduma za upimajiwa kiwango cha sukari kwenye damu (RBG),shinikizo la damu (BP),uwiano wa uzito na urefu wa mwili (BMI) na ushauri wa kitaalamu ulitolewa na madaktari,wakati wa mapokezi ya mwenge wa uhuru kwenye viwanja vya shule ya msingi Somanga-Kilwa.Picha na Paul Marenga-NHIF LINDI

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad