.jpg)
Baadhi ya Watoto Mayatima wanaoishi katika Kijiji Cha Jaribu - Rufiji walipopiga picha ya Pamoja na Wajumbe wa Taasisi ya Kalamu Foundation baada ya Kukabidhiwa vyakula Mbali Mbali na Magodoro 25 kwa ajiri ya Kituo cha watoto yatima Kijijini Hapo.
Wajumbe wa Taasisi ya kijamii ya Kalamu Education Foundation walipokuwa wakimkabidhi Binti Simba Vifaa Mbali Mbali pamoja na Nguo, Sabuni, Mashuka na Viatu kwa ajiri ya Kituo Cha Jaribu Orphans Center wilayani Rufiji Mkoa wa Pwani kwa ajiri ya Mwezi Mtukufu wa Ramadhan.
Mjumbe
wa Taasisi ya Misaada ya Kibinaadam Ya Kalamu Education Foundation Mh.
Asha Mtwangi (Kushoto) ambae ni Mjumbe wa Bunge la Katiba Akimsikiliza
Kwa Makini Bint Simba wa Kituo Cha Jaribu Orphans Center akielezea
Maisha ya Kila Siku ya watoto wa Kituo Hicho wa Jamii ya Kijiji Cha
Jaribu Rufiji - Pwani. Alisema "laiti taasisi mbali mbali zingetembelea
huku vijijini kama mlivyofanya nyinyi ambako hali zetu ni ngumu zaidi,
wananchi wengi tungefarijika sana hasa kipindi hiki cha mwezi Mtukufu".
Baadhi
ya wanakamati wa Taasisi ya Kalamu Education Foundation wakiteta jambo
na Bint Simba ambaye ni Bibi Mleze wa Kituo Cha watoto yatima Kijiji cha
Jaribu. Bint Simba Alishukuru sana kwa Taasisi ya Kalamu Foundation kwa
kuwajali wananchi wa vijijini kipindi hiki Cha Mwanzo wa Mwezi Mtukufu
wa Ramadhani.
No comments:
Post a Comment