Mtu mmoja amethibitishwa kufariki Dunia na wengine zaidi ya 20 kujeruhiwa vibaya baada ya moja ya Barabara
iliyokuwa kwenye matengenezo kukatika katika mji wa Belo Horezonte karibu na eneo lenye shughuli
nyingi la Lagoa da Pampulha,nchini Brazil.
Barabara
hiyo ipo kilometa 3 kutoka Mineirao
Stadium,uwanja uliotumika kwa mechi mbali mbali za kombe la dunia na
utatumika kwenye nusu fainali ya Kombe la Dunia 2014.
Barabara hii ilikuwa ni moja ya
kiungo kinachounganisha uwanja wa mpira na uwanja wa Kimataifa wa
Ndege. Barabara hiyo ni mpango wa mbasi ya mwendo kasi ambayo ilisemekana ingekuwa tayari kutoa huduma wakati wa mashindano ya Kombe la Dunia.
Maafisa
wa kikosi cha uokoaji nchini humo wakiendelea na kazi ya kuyanasua magari yaliyonasa baada ya kuangukiwa na Barabara hiyo,ambapo wamethibitisha kwamba Dereva wa basi hili ndie aliefariki Dunia katika
tukio hilo la kuanguka kwa barabara hiyo ya Juu (Fly Over) kwenye mji wa Belo Horizonte,Brazil.
Kazi ikiendelea. Picha na AFP/Reuters
No comments:
Post a Comment