Umoja wa kikundi cha wanawake cha Airtel Divas leo kimetembelea kikundi cha sauti ya wanawake walemavu Tanzania (SWAUTA) katika banda lao lililopo katika maonyesho ya Sabasaba jijini Dar es Saalam
Airtel Divas wamefanya hivyo hivyo ikiwa ni muda mfupi tu tangu walipofanya harambee ya kukiwezesha kikundi hicho kupata fedha za kulipia banda katika viwanja vya maonyesho ya 38 ya kimataifa maarufu kama Sabasaba ili nao kuonyesha bidhaa zao kwa watanzania
Akiongea wakati wa ziara hiyo, mwanachama wa Umoja wa wanawake wa Airtel na Meneja Huduma kwa jamii Hawa Bayumi alisema” Airtel Divas tunayofuraha kuona tumeweza kuwasaidia kina mama wenzetu kutimizia lengo lao na kuwapa nafasi yakuweza kuonyesha ubunifu wao uwezo wao na kazi zao za mikono kwa washiriki na wateja wa ndani na wanje wanaotembelea maonyesho haya ya Sabasaba.
Ni matumaini yetu kuwa fulsa hii ya kuonesha na kujitangaza hapa saba saba itawawezesha kufikia malengo yao ya kutanua wigo wa biashara zao na kupata masoko na kuuza bidhaa zao kwa wingi zaidi. Tunatoa wito kwa watanzania kujitokeza na kuwaunga mkono kina mama hawa katika banda lao lililoko Benjamini Mkapa.
Kwa upande wake Mwanachama wa Umoja wa sauti ya walemavu Tanzania Bi Adelina Mluge Alisema “Tunawashukuru sana Airtel kwa kutuwezesha kuwepo katika mazingira mazuri ukilinganisha na ilivyokuwa na miaka iliyopita. mpaka sasa tumeweza kupata wateja wengi wakipita hapa kuona na kununua bidhaa zetu kwa wingi. Tunategemea kufanya vyema katika maonyesho ya mwaka huu kutokana na maboresho haya na hivyo basi tunaishukuru sana kampuni ya Airtel kwa kujitolea kutusaidia.
Airtel kupitia huduma zake za jamiii imeweza kuwafikia jamii na kuwawezesha kupata huduma muhimu hususani katika elimu, Airtel kwa kupitia Divas Airtel inaendelea kusaidia jamii katika maeneo mbalimbali ikiwemo kina mama hawa wa umoja wa sauti ya walemavu Tanzania.
Wanachama
wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,
Meneja wa Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi (kushoto), Afisa Uhusiano, Jane
Matinde (wa pili kushoto), na Afisa mauzo, Rachael Mboya (kulia),
wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha Sauti ya Wanawake
wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni, walipotembelea Banda la
Swauta, lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya
Kimataifa (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana.
Airtel Divas ilikiwezesha kikundi hicho, kupata pesa kwa ajili kulipia
banda hilo.
Mwanachama
wa Kikundi cha Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha
Kinondoni, Adelina Mluge (kulia), akitoa maelezo kuhusu bidhaa
zinazouzwa na kikundi hicho kwa Wanachama wa Kikundi cha Wanawake
wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’, (kutoka kushoto), Afisa
Mauzo, Rachael Mboya, Afisa Uhusiano, Jane Matinde na Meneja wa Huduma
kwa Jamii, Hawa Bayumi, walipotembelea Banda la Swauta, lililopo katika
Uwanja wa Maonyesho ya 38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), barabara
ya Kilwa jijini Dar es Salaam jana. Airtel Divas ilikiwezesha kikundi
hicho, kupata pesa kwa ajili kulipia banda hilo.
Wanachama
wa Kikundi cha Wanawake wafanyakazi wa Airtel Tanzania ‘Airtel Divas’,
Meneja wa Huduma kwa Jamii, Hawa Bayumi (kulia), na Afisa Uhusiano, Jane
Matinde (kushoto), wakichagua bidhaa zilizotengenezwa na Kikundi cha
Sauti ya Wanawake wenye Ulemavu Tanzania (SWAUTA) cha Kinondoni,
walipotembelea Banda la Swauta, lililopo katika Uwanja wa Maonyesho ya
38 ya Biashara ya Kimataifa (Sabasaba), barabara ya Kilwa jijini Dar es
Salaam jana. Airtel Divas ilikiwezesha kikundi hicho, kupata pesa kwa
ajili kulipia banda hilo.
Baadhi
ya wafanyakazi wa Airtel wakiwa katika picha ya pamoja na kikundi
SWAUTA katika banda lao kwenye maonyesho ya Sabasaba, ambapo Airtel
Divas imekiwezesha kikundi hicho kuwa na banda katika maonyesho hayo.
Afisa
Mauzo wa Airtel , Rachael Mboya,akiangalia kazi ya kikundi cha ulemavu
ikiwemo kushona na uwezo wa kusoma vitabu mbalimbali vilivyopo katika
banda lao wakati wanawake wa Airtel Divas walipotembelea banda lao
katika maoenyesho ya sabasaba.
No comments:
Post a Comment