Meneja wa Mauzo wa Kampuni ya Bia nchini(TBL), Robert Kaziwa (kushoto)akimkabidhi mwakilishi
wa wa kikundi cha Magereza Arts Group zawadi ya kitita cha Shilingi 600,000/= mara baada ya
kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Balimi Kanda ya Ziwa ngazi za mikoa Mkoa Mkoa
wa Tabora mwishoni mwa wiki.
Baadhi ya wacheza ngoma wa Magereza Arts Group wakishangilia na kitita cha Shilingi 600,000/
=mara baada ya kuibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya Balimi Ngoma Mkoa wa Tabora
yaliyomalizika mwishoni mwa wiki Mkoani humo.
Na Mwandishi Wetu.
FAINALI za mashindano ya Ngoma za Asili ngazi ya mikoa zijulkanazo kama “Balimi Ngoma Festival
2014” Tabora na Shinyanga wamepata wawakilishi watakaowakilisha mikoa hiyo katika fainali za Kanda
ya Ziwa zinazotarajiwa kufanyika Augusti 16,2014, Mkoani Mwanza.
Mkoa wa Tabora kikundi cha Magereza Arts Group kilifanikiwa kutwaa ubingwa wa Mkoa huo
na hivyokuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 600,000/= na tiketi ya kuwakilisha kwenye fainali za
Kanda.Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Bugobogobo na hivyo kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
500,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha mkoa kwenye fainali za Kanda.Jumla ya vikundi 8 ambavyo ni
pamoja na JKT,Hekima,Uvikuja,Wembe Group,Hiari ya Moyo,Zugo Group.
Mkoa wa Shinyanga kikundi kilichofanikiwa kuchukua Ubingwa ni Mabulo ya Jeshi ambacho
kilizawadiwa fedha taslimu Shilingi 600,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga
kwenye fainali za Kanda.Nafasi ya pili ilichukuliwa na kikundi cha Wananguli Bugumbagu ambao
walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 500,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha Mkoa wa Shinyanga
kwenye fainali za Kanza Mkoani Mwanza.Jumla ya vikundi 10 Shinyanga vilishiliki ambavyo ni
pamoja na Wagoyangi Bugumbagu,Buzori Usule,Bagoyangi Usule,Busumbi,Kadete Chibe,Wagoyangi
Maswa,Wananguli Bugimbagu na Uswezi Usule.
Akizungumza na kwa nyakati tofauti Meneja matukio wa Kanda ya Ziwa, Erick Mwayela alisema Sababu
msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa
Kitanzania.
Mwayela aliongeza pia kuwa wao Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila
kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager pamoja na vinywaji vyote vya Kampuni ya Bia
Tanzania(TBL).
Fainali za Kanda za mashindano ya Balimi Ngoma zinatarajiwa kufanyika August 16,2014 jijini Mwanza
kwa kushilikisha vikundi viwili viwili kutoka Tabora, Shinyanga, Bukoba, Musoma na Wenyeji wa
mashindano Mwanza.
No comments:
Post a Comment