HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 18, 2014

MJUMITA Yaokoa misitu ya Liwale baada ya kutoa elimu shirikishi kwa jamiii

Na Abdulaziz ,Lindi

Mtandao wa Jamii wa Usimazi wa misitu Tanzania (MJUMITA) wamekuwa wakitoa elimu ya utawala bora katika vijiji 24 vinavyozunguka msitu wa Angai kuanzia mwaka 2011 kwa ufadhili wa Limas (lindi and masasi agribusiness support) Mjumita wamekuwa wakitoa elimu hiyo katika hivyo ikiwemo Uraghabishi ,utawala bora, Usimamizi shirikishi wa misitu,Uongozi na Utawala bora huku Elimu ikitolewa kwa jamiii za vitongoji juu ya uwezeshaji na utunzaji wa misitu kwa manufaa ya jamiii zilizo katika vitongoji na Vijiji wilayani Liwale.

Akiongea na Globu ya Jamii ,Bw Frank Munuo mwakilishi wa Mjumita wilayani humo alieleza kuwa Vijiji 3 miongoni mwa vijiji 24 vilivyo katika msitu wa Angai wilayani Liwale vitaanza uvunaji mwishoni mwa mwezi huu(June)baada ya kukamilisha michakato yote hatimaye kufikia hatua ya uvunaji Vijiji hivyo ni Mtawatawa, Kitogoro na Litohu vimefikia hatua hiyo baada ya elimu iliyotolewa na ikiwa ni hatua ya kipekee kwa vijiji kuanza kufaidika na misitu ya vijiji kwani kupitia Uvunaji huo asilimia 95% ya mapato yatakuwa ni kwa ajili ya kijiji na asilimia 5% ni kwa Halmashauri ya wilaya kwa ajili ya kusaidia kutoa huduma pale watakapohitajika kufanya hivyo.

Aidha Frank alibainisha pia Kufikia hatua hiyo yaa ya vijiji hivyo 3 kuanza uvunaji ni hatua ya kipekee kwa wanajamii kuanza kunufaika na raslimali hizi za misitu moja kwa moja imetokana na Mafunzo kwa vijiji hivyo 24 mafunzo ambayo yamesaidia utunzaji wa Misitu pamoja na kumaliza migogoro ya Vijiji ikiwemo ya Mipaka na na Utawala Bora.

Kwa Upande wake,Mkuu wa Wilaya ya Liwale,Ephraim Mmbaga akiongea na waandishi wa habari waliotembelea wilaya hiyo alieleza kuwa Usiri wa jamiii na kuoneana haya ndio changamoto kubwa inayoathiri maendeleo ya wilaya hiyo huku raslimali zikinufaisha wachache.

Akiongelea mpango unaoendelezwa kwa Usimamizi wa Mjumita na Limas,Mmbaga amesema ameridhishwa na Asasi hizo kwa kusaidia kutoa elimu kwa jamiii kutunza misitu yao ili wanufaike na rasilimali hizo hulu akibainisha uelewa uliopo Vijijini baada ya kupewa mafunzo ya Utawala Bora ambapo kwa sasa vijiji vinakutana kupanga mipango shirikishi ya Maendeleo Ikiwemo kubainisha mapato na matumizi,Usawa wa kijinsia,Huduma za Jamii pamoja na kulinda Misitu baada ya kuelewa manufaa yatakayopatikana
Wananchi wakiendelea kucheza pamoja na katibu wa kamati ya maliasili huku kina mama na kina baba wakisubiri kwa hamu mkutano mkuu wa tar 30/6/2014 kujua mbivu na mbichi kuhusiana na vifaa na mbao zilizotaifishwa baada ya kukamatwa msituni.
Wananchi wa kijiji cha Mahonga wakiendelea kujadili wakiwa kwenye vikundivikundi huku wakisubiri kuletwa kwa chainsaw iliyokamatwa baada ya wananchi kuazimia iletwe kijijini na ikabidhiwe kwa Mtendaji wa kijiji ifikishwe kwa Idara ya misitu ya Halmashauri hiyo tar 13/6/2014 kutokana na Uharibu mkubwa unaofanywa kwa kutumia mashine hiyo kuteketeza misitu kwa haraka na kuharibu hifadhi ya misitu ya Vijiji vinavyozunguka Misitu ya Angai wilayani Liwale.
Mwenyekiti wakijiji cha Mahonga ambayeyupo mstari wa mbele toka kukamatwa kwa mbao 6/6/2014 yupo eneo la hifadhi akisaidianana kamati ya maliasil ikuhakikisha mbao zipatazo 100 zinafika kijijini baada yaTrekta walilopanga kusafirishia mbao hizo kuharibika ambapo tayari ulinzi umewekwa kudhidhibiti.
Mwenyekiti wa kitongoji wa kijiji cha Ngunja akisoma taarifa ya Utekelezaji ya Kitongoji chake kwa wananchi wakati Mkutano mkuu maalumu wa kijiji cha Ngunja Kilichopo kata ya Ngongowele wilayani Liwale.
Mwana mama machachari ambae pia ni Mtathmini wa Utawala Bora toka kijiji cha Ngunja (Bi:SomoeNkoma)akizungumzia utawala bora baada ya jamiii ya Kijiji hicho baada ya Kupewa mafunzo ya Utawala bora yaliyotolewa na Asasi za Mjumita na Limas Hivi karibuni.
Katibu wa kamati ya maliasili akiwasili na mashine ya kukatia misitu(Chain saw) katika mkutano mkuu maalumu wa kijiji wa uliofanyika katika uwanja wa mikutano katika kijiji cha Mahonga ambapo taarifa.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad