HABARI MPYA

Home Top Ad

Post Top Ad

Wednesday, June 18, 2014

Hali ya Mto Janga jijini Mbeya inahatarisha maisha ya wananchi

Kutokana na watu mbalimbali kutupata taka ovyo katika mto wa janga katika Uliopo eneo la Ilolo,Halmashauri ya Jiji la Mbeya,imekua ni hatali hasa kwa wakazi wa eneo hilo kutokana na hali ilivyo kwenye mto huo,kwani watu mbalimbali hutumia maji hayo kwa matumizi mbalimbali kama kumwagilia mboga za majani kufyatulia tofali na matumizi mengine yenye kukidhi haja za nyumbani,Kamera ya Mtaa kwa Mtaa Blog ilizungulia eneo hilo na kukutana na Mwenyekiti wa mtaa huo nae akazungumzia tatizo hilo na kuwataka wakazi wa maeneo hayo kufanya usafi wa pamoja katika mto huo.

Hali hiyo inahatarisha maisha ya wakazi wa eneo hilo hasa kwa magonjwa ya milipuko kama vile Kipindupindu na mengine mengi.Picha na Fadhil Atick,Mbeya. 
Mmoja wakazi wa eneo hilo ambaye jina lake halikuweza fahamika mara moja akichota maji katika mto huo ili hali si salama kwa matumizi ya Binadamu.
Taswira mbali mbali za namna mto huo unavyoonekana.

No comments:

Post a Comment

Post Bottom Ad