Mkurugenzi wa Kampuni ya Msama Promotions, Alex Msama
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, kuhusu maandalizi
ya tamasha la Pasaka litakaloanza kutimua vumbi April 20. (Picha na Francis
Dande)
Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi ya tamasha Na Francis Dande
MALKIA wa muziki wa Injili nchini Afrika Kusini, Rebecca
Malope, ni miongoni mwa wasanii watakaotumbuiza kwenye Tamasha la Pasaka mwaka
huu.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam, Mwenyekiti wa Kamati ya Maandalizi
ya tamasha hilo ,
Alex Msama, msanii huyo amepata kura nyingi kutoka kwa mashabiki
waliompendekeza.
“Tunashukuru kwamba baada ya mapendekezo ya mashabiki
tuliwasiliana na Rebecca ambaye ameonesha uungwana wa hali ya juu na
kutukubalia ombi letu. Lakini pamoja na kukubali ana ratiba ya maonesho sehemu
nyingine huko kwao, hivyo ametuambia hatatumbuiza katika mikoa yote ambayo
tamasha litafanyika mwaka huu, hivyo tutaangalia wapi tumpangie kulingana na
ratiba yake,” alisema Msama na kuongeza.
“Lakini niwahakikishie mashabiki wetu kwamba, msanii huyo
tutakuwa naye na sasa ni suala la Kamati ya Maandalizi kuona ratiba yake ilivyo
na kisha nasi tumweke kwenye ratiba yetu ili mashabiki wafurahi.”
Rebecca amewahi kutamba na albamu za ‘Saturday Nite’
aliyoitoa Januari 1, 2009, ‘Hlala Nami’ Novemba 11, 2003, ‘Siyabonga’ Desemba
21, 2000, ‘Free at Last’ Novemba 18, 1997, ‘African Classics’ Mei 5, 2009 na ‘Greatest
Hits’ Januari 10, 2006.
Wasanii wengine watakaotumbuiza kwenye tamasha hilo ambao
tayari wameshathibitisha ni Upendo Nkone, John Lissu, Upendo Kilahiro na Rose
Muhando wote wa Tanzania na Sarah K wa Kenya.
No comments:
Post a Comment