Mkutano wa nane wa maajadiliano ya wazi kuhusu maandalizi ya malengo mpya ya maendeleo endelevu baada ya 2015 ( SDGs) umekamilika siku ya Ijumaa hapa Makao Makuu ya Umoja wa Mataifa.
Katika Mkutano huu wa wa wiki moja wajumbe walijadiliana na kubadilishana mawazo kuhusu mada kadhaa ambazo ziliwasilishwa mbele yao kuangalia ni kwa namna gani zinaweza kuwa sehemu ya malengo hayo mapya ya maendeleo endelevu.
Mada hizo zilihusu masuala ya Bahari, Misitu na Viumbe hai, Usawa wa Jinsia na uwezeshwaji wa wanawake, uzuiaji wa machafuko, uimarishaji wa amani , ujenzi wa amani baada ya machafuko, utawala wa sheria na utawala bora.
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni kati ya Mataifa 30 yaliyokuwa yamechaguliwa kuwa wajumbe wa majadiliano hayo ya wazi ( Open Working Group). na Imeshiriki kikamilifu tangu mkutano wa kwanza hadi huu wa mwisho
Balozi Celestine Mushy, Mkurugenzi, Idara ya Ushirikiano wa Kimataifa, akizugumza katika mkutano huo wa mwisho wa maandalizi ya malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015, Balozi Mushy ndiye aliyeongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano huo. Pembeni ni Bw. Noel Kaganda Afisa wa Uwakilishi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Wajumbe wakifuatiali mchango wa Tanzania uliowasilishwa na Balozi Mushy kuhusu uzuiaji wa machafuko, uimarishaji wa amani, ujenzi wa amani baada ya machafuko, utawala wa sheria na utawala bora.
Sehemu wa washiriki wa mkutano wa mwisho wa maandalizi ya malengo mapya ya maendeleo endelevu baada ya 2015.jpg)
.jpg)
Washiriki wengine wakifutalia kwa makini majadiliano hayo

.jpg)
.jpg)
.jpg)
No comments:
Post a Comment