MAREHEMU DR. CLEOPHAS KENTE RUTABINGWA
KUZALIWA 18/1/ 1952 – KIFO 17/1/2014
Leo tarehe 27/02/2014 zimetimia siku Arobaini (40) tangu Mwenyezi Mungu akuite nyumbani, tarehe 17/1/2014.
Ilikuwa siku ya majonzi makuu katika familia yetu kifo kilitokea katika Hospitali ya Mbweni Dar es Salaam, ulipoumwa na tumbo.
Unakumbukwa sana na familia yako, Mama yako mzazi Magreth Kente , Mke wako Praxeda Rutabingwa, watoto wako Andrew, Antidius, na Magreth, ndugu jamaa, majirani, marafiki, wanachama wenzako MAJIRANI SOCIAL CLUB, UJIRANI MWEMA TANGIBOVU- MBEZI BEACH, JUMUIYA YA KRISTO MFALME, KIGANGO CHA MT. THOMAS MORE, PAROKIA YA MT. GASPAR DEL BUFALO MBEZI BEACH, DAR ES SALAAM, CHUO CHA MT. AUGUSTINE, CHUO CHA MZUMBE, na wengine wote, wanakukumbuka kila mmoja kwa namna ya pekee.
Misa ya kumuombea Marehemu itafanyika tarehe 1/3/2014 siku ya Jumamosi asubuhi saa 12.45 katika Kigango cha Mt. Thomas More Mbezi Beach.
Mwenyezi Mungu ailaze roho yako mahali pema peponi, kwa watakatifu wake. Bwana alitoa na ametwaa jina lake lihimidiwe milele.
Amen.
No comments:
Post a Comment