Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhe. Mathias Chikawe akipokea hati ya maboresho ya Jeshi la Polisi, mpango kazi wa Jeshi la Polisi Pamoja na kitabu chenye miongozo ya Jeshi la Polisi kutoka kwa Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini, IGP Ernest Mangu Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam leo,alipoanza kufanya ziara katika idara za Wizara aliyokabidhiwa kuiongoza hivi karibuni.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mathias Chikawe (aliesimama), akizungumza na maofisa wakuu waandamizi wa Jeshi la Polisi nchini, Makao Makuu ya Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam alipoanza kufanya ziara katika idara za Wizara aliyokabidhiwa kuiongoza hivi karibuni. Kulia ni Naibu Waziri Mambo ya Ndani Mhe. Pereira Silima na kushoto ni Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Ernest Mangu.
Waziri
wa Mambo ya Ndani ya Nchi,Mhe. Mathias Chikawe (katikati) akiwa na
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani, Mhe. Pereira Silima na Mkuu wa Jeshi la
Polisi Nchini,IGP Ernest Mangu pamoja na maofisa wakuu wa Jeshi la
Polisi wakiimba wimbo wa Maadili wa Jeshi la Polisi wakati Waziri
Chikawe alipofanya ziara katika idara ya Polisi Makao Makuu ya Jeshi la
Polisi Dar es Salaam leo.Picha Na Hassan Mndeme-Jeshi la Polisi.



No comments:
Post a Comment