Katika kipindi cha sikukuu ya Mwaka mpya Mkoani Dodoma yamejiri matukio kadhaa. Katika tukio la pili, mnamo tarehe 31/02/2013 saa 20:00hrs usiku katika kijiji cha Ndalibo Kata ya Mtanana Wilaya ya Kongwa Mkoa wa Dodoma.
Mtu aliyefahamika kwa jina la KAMOTA s/o CHIMASI, 50yrs, Mkagulu, Mkulima na mfugaji, mkazi wa Ndalibo, aliuwawa kwa kupigwa risasi mgongoni kwa kutumia bunduki aina ya Gobore na watu wasiofahamika wakati akiwa nje ya zizi akihesabu ng’ombe wake. Katika tukio hilo hakuna kilichoibiwa na Chanzo mauaji hayo bado hakijafahamika.
Watu watatu wanashikiliwa na Polisi kwa mahojiano pamoja bunduki aina ya gobore na Upelelezi unaendelea kubaini chanzo na sababu ya tukio hilo.
Katika tukio la tatu, mnamo tarehe 01/01/2014 majiraya saa 01:00hrs usiku huko eneo la barabara ya 11 Kata ya Madukani Manispaa ya Dodoma, duka la vifaa vya Kielectronic linalomikiwa na MARRY d/o RICHARD, 32yrs, Mchaga, Mfanyabiashara mkazi wa Nkuhungu Dodoma lilivunjwa na mali mbalimbali zikiwemo simu 150, digital camera 6, redio Sub –hoofer 7 na pasi 5 vyote vikiwa na thamani ya Tsh. 7,665,000/=.
Mbinu iliyotumika ni kuvunja kwa kukata Seilingbaord kutokea upanda wa nyumba ya kulala wageni iitwayo NASIBU chumba namba 2 na kutokeza dukani kwa kuwa duka hilo limeungana na nyumba ya wageni. Hakuna mtu aliyekamatwa na upelelezi wa tukio unaendelea.
Katika tukio la nne mnamo tarehe 01/01/2014 majira ya saa 12:00hrs mchana katika kitongoji cha Mhuti kijiji cha Chigongwe Manispaa ya Dodoma. Bibi kizee aliyefahamika kwa jina la EMMY d/o MJENZI @ MCHIMBU, 106yrs, mgogo, Mkazi wa Mtaa wa Mhuti kijiji cha Chigongwe, alifariki dunia kwa kujinyonga chumbani kwake kwa kutumia kamba ya mbuyu iliyosokotwa. Marehemu huyo aliwahi kujaribu kujinyonga mara mbili mwezi Mai,2013 na mwezi Novemba, 2013 lakini aliokolewa. Sababu ya kujinyonga ni kuchoka kuishi kwa muda mrefu. Uchunguzi zaidi wa tukio hilo unaendelea.
Tukio la tano mnamo tarehe 31/12/2013 Mjaira ya 21:00hrs Katika mtaa wa Mbabala “A” kijiji cha Mbabala Manispaa ya Dodoma, mtoto aliyefahamika kwa jina la IRENE d/o SIMPHORIAN, 7yrs, mgogo, mwanafunzi darasa la kwanza S/Msingi Mwenge, alipotea katika mazingira ya kutatanisha nyumbani kwake baada ya kuachwa pekeyake na wazazi.
Alipatikana mnamo tarehe 01/01/2014 saa 17:00hrs akiwa amefariki dunia eneo la pori la jirani umbali mita 300 kutoka nyumbani kwaopia ni jirani na Kanisa la Anglikana. Hakuna mtu aliyekamatwa kuhusiana na tukio hilo, uchunguzi wa mwili wa marehemu unafanyika na upelelezi zaidi juu ya tukio hilo unaendelea.
Jeshi la Polisi linaendelea kusisitiza wananchi wake kutojichukulia sheria mkononi na badala yake watoe taarifa Polisi mapema ili kuokoa uhai wa watu na malizao. Aidha wafanyabiashara wahakikishe mali zao zinakuwa katika mazingira salama na kutoruhusu mianya kwa wahalifu kuvunja na kuiba.
SUZAN KAGANDA -ACP
KNY:
KAMANDA WA POLISI MKOA WA DODOMA


No comments:
Post a Comment