WAKATI maandalizi yam bio ndefu za Uhuru, Uhuru Marathon, yakiwa yamekamilika zawadi kwa washindi zimetangazwa upya pale mshindi wa mbio ndefu za kilomita 42 kwa upande wa wanaume na wanawake akiondoka na Sh milioni 2.
Huku mshindi huyo akiondoka na fedha hizo, kwa upande wa mbio za kilomita 21 kwa wanaume na wanawake kila mmoja ataondoka na Sh milioni 1, hivyo kuongeza chachu ya mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika kesho kwa kuanzia na kumalizikia katika Viwanja vya Leaders, vilivyopo Kinondoni, Dar es Salaama.
Akizungumza na waandishi wa habari jana kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki, Kaimu Mkuu wa Mkoa, Sophia Mjema alisema, wana faraja kubwa kwa maandalizi ya mbio hizo kukamilika na hivyo kutimiza azma ya kudumisha uhuru, amani, umoja na mshikamano uliopo miongoni mwa Watanzania.
“Tunachukua fursa hii pia kutoa shukrani za dhati kwa Rais Jakaya Kikwete kwa kukubali kwake kushiriki mbio hizo kwa mbio za kilomita 3. Hii inadhihirisha jinsi Rais Kikwete alivyoguswa mno na suala la kupigania amani, umoja na mshikamano miongoni mwetu.
“Pia tunatangaza rasmi kwamba kutakuwa na wanariadha wa mataifa mbalimbali waliojitokeza kushiriki mbio hizo ambao wengi wao wanatoka Tanzania, Uganda, Kenya, Afrika Kusini, Ethiopia, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Malawi, Marekani, Ujerumani, Jamaica, Urusi, China, Japan, Venezuela, Comoro, Nigeria, Italia, Canada, Madagascar na Uturuki.
“Tunafurahi kutangaza kwamba mmoja wa wanariadha hao ni bingwa wa dunia wa marathon kwa upande wa wanawake, Edna Kiplagat wa Kenya, aliyetwaa taji la dunia mwaka 2011 kule Korea Kusini na mwaka 2013 katika mashindano yaliyofanyika Moscow, Urusi.
“Mbali na Rais Kikwete pia tuna viongozi mbalimbali wa kitaifa ambao wanatarajiwa kushiriki mbio hizo, huku wengine wakianza kuwasili leo wakiwemo pia wanariadha watakaowasili leo na kesho kwa ajili ya kushiriki mbio hizo zinazotarajiwa kufanyika Jumapili.
“Tunapenda kuchukua fursa hii kutangaza rasmi kila kitu kimekamilika kwa ajili yam bio hizo, ikiwa pamoja na kutengeneza njia itakayotumiwa na wanariadha kuanzia wa kilomita tatu hadi kilomita 42, hii ikiwa pamoja na kuweka vituo maalumu kwa ajili ya maji kwa wanariadha wetu,” alisema.
Kuhusu zawadi alisema, jumla ya Sh milioni 13.6 zitatolewa kama zawadi ambapo mbali na hizo zilizotajwa hapo juu mshindi wa pili kwa wanaume na wanawake kwa kilomita 21 kila mmoja ataondoka na Sh 700,000 huku kilomita 42 wakiondoka na Sh milioni 1 kwa kila mmoja.
Mshindi wa tatu kilomita 21 kwa wanaume na wanawake kila mmoja atapata Sh 500,000 na kilomita 42 watapata Sh 600,000 washindi wa nne kwa kilomita 21 na 42 kwa wanawake na wanaume kila mmoja ataondoka na Sh 300,000 wakati yule atakayeshika nafasi ya tano kwa kilomita 21 wanawaume na wanawake atapata Sh 150,000 na kilomita 42 itakuwa Sh 200,000 huku walemavu kumi watakaoshiriki kila mmoja atapewa Sh 100,000.
Naye Katibu wa Kamati ya Mbio hizo, Innocent Melleck alisema pia maandalizi kwaajili ya tamasha la mkesha wa Uhuru yamekamilika vyema na wasanii 12 wanatarajiwa kutumbuiza usiku huo wakiongozwa na Roma Mkatoliki, Joh Makini, Mrisho Mpoto, Nick wa Pili, G Nako, TMK Wanaume, Msondo Ngoma, Twanga Pepeta, Mfalme Siboka na wengineo na kiingilio kitakuwa Sh 2,5000. Tamasha litafanyika Viwanja vya Leaders.
“Tumejipanga pia kwa ulinzi wa kutosha kuhakikisha kuwa ulinzi wetu na mali zetu unakuwa wakutosha kwa kipindi chote hivyo hakuna haja ya kuwa na hofu yoyote juu ya usalama wa mali zet,” alisema huku akifafanua kituo cha televisheni cha TBC na kile cha radio TBC Taifa watarusha moja kwa moja mbio hizo.
Mbio za Uhuru zimedhaminiwa na GrandMalt, Konyagi, Kibuku, Mwananchi Communications, Sayona, CocaCola, KAPARI, Clouds FM, Uhuru FM, TBC 1, TBC Taifa, Integrated Communications, Night Support, Tindwa Medical, Michuzi Media Group,Forever Living na SamSung.

No comments:
Post a Comment