Afisa Mazingira Mkuu kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Bw. Japhet Kanizius, Akimkaribisha Mgeni Rasmi Bi. Magdalena Mtenga, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira) kufungua rasmi warsha ya mafunzo kwa mafundi wa kuhudumia majokofu na viyoyozi kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa. Mafunzo haya yanafanyika katika Hotel ya Mbeya Paradise Inn, Jijini Mbeya.
Sehemu ya washiriki kutoka Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini wakifuatilia hotuba ya ufunguzi kutoka kwa Mgeni Rasmi, Bi. Magdalena Mtenga, Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Mazingira).
Washiriki wa Warsha ya mafunzo kwa mafundi wa kuhudumia majokofu na viyoyozi kutoka Mikoa ya Mbeya, Iringa, Ruvuma na Rukwa wakiwa katika picha ya pamoja na Mgeni rasmi Bi. Magdalena Mtenga Mkurugenzi Msaidizi Ofisi ya Makamu wa Rais (Waliokaa - kwanza kushoto). Mafunzo haya yanafanyika katika Hotel ya Mbeya Paradise Inn, Jijini Mbeya.
No comments:
Post a Comment